Blogger Widgets

March 20, 2014

Msani wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford, amefunguka jinsi pombe ilivyomuathiri


DIVA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford, amefunguka kuwa ameamua kuacha pombe kwa sababu ameona haina faida yoyote kwake zaidi ya kumzeesha na kumfanya aonekane kama mama mtu mzima.
Shamsa Ford.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, juzikati jijini Dar es Salaam, Shamsa alisema: “Nilikuwa napiga sana mtungi, yaani nilikuwa nikipata nafasi ya kunywa, napiga balaa lakini naona hakuna cha maana, sanasana nimeambulia kuharibu umbo langu tu,” alisema Shamsha na kuongeza:
 
“Nimeamua kuachana nayo kabisa. Haina faida na mimi. Achilia mbali kupoteza mvuto wangu lakini pia namaliza fedha nyingi, sitaki, nimesema sitaki tena pombe.”