Blogger Widgets

March 10, 2014

Nora Nae Ataka Kiki kwa Hii Habari Ambayo Imewachanganya watuMWIGIZAJI mkongwe Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ amefunguka kuwa anakerwa na matapeli walioibuka ambao wanawatapeli wasanii wa kike wakiwadanganya kwamba wanawachezesha filamu kumbe ‘changa la macho’.
 
Nuru Nassoro ‘Nora’.
Akistorisha na paparazi wetu, Nora alisema hivi karibuni alikutwa na mkasa huo baada ya kupigiwa simu na wanaume wawili waliodai kwamba wana filamu yao hivyo wanataka wamchezeshe kama mhusika mkuu (main character) lakini baada ya kukutana nao, mazungumzo yao yalikuwa tofauti.
“Walinikera sana, waliniambia kwamba wanataka kunichezesha filamu lakini nilipoenda kuonana nao walibadili mazungumzo na kuanza kunitaka kimapenzi, ujinga mtupu, niliwakatalia,” alisema