Blogger Widgets

March 6, 2014

Soma Sababu aliyoitoa Msanii Nazii wa Necessary Noice Mpaka Kufikia Kuachana na Mume wake

Nazizi wa Kenya aachana na mume wake baada ya miaka mitano ya ndoa !!!!
 Msanii wa kundi la Necessary Noise la Kenya Nazizi Hirji amethibitisha kutengana na mume wake baada ya ndoa yao kudumu kwa takribani miaka mitano.
Naziz

Nazizi, mumewe na mwanao
Nazizi alithibitisha juu ya taarifa hizo alipofanya mahojiano na Nairobi News na kuongeza kuwa hawezi kutoa taarifa zaidi lakini ni kweli ndoa yao imefikia ukingoni.

“Siwezi kutoa taarifa zaidi kuhusu hilo, lakini ninaweza kukuthibitishia kuwa ndoa imevunjika.” Alisema Nazizi.
Nazizi-2
Aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ngumu kwake kuishi Lamu yalikokuwa makazi ya familia yake na mumewe Mtanzania aitwaye Vinny, hivyo imemlazimu kurejea Nairobi ambako familia yake iliko.

“Ilikuwa ni vigumu kuishi Lamu, nilihitaji kurudi Nairobi ambako wanafamilia wangu wote wako”.

Nazizi alimalizia kwa kusema yeye na aliyekuwa mume wake ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume bado wanazungumza licha ya ndoa yao kuvunjika.

Source: Nairobi Wire