Blogger Widgets

March 22, 2014

Soma Uamuzi wa Boss wa Tip Top Connection Babu Tale juu ya Ombi la dogo janja kurudi Tip Top

Baada ya Dogo Janja kuuomba msamaha kupitia vyombo vya habari uongozi wa Tip Top Connection na Madee aliyemtoa Arusha, Boss wa Tip Top Connection Babu Tale ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa anataka rapper huyo aseme ukweli wa yote aliyoyasema awali baada ya kutoka Tip Top.
“Babu Tale ameweka wazi vipengele ambavyo anataka Dogo Janja aviweke sawa.
“Dogo anatakiwa aseme kama kweli aliibiwa, kama kweli alidhurumiwa na kama kweli hajawahi kuishi nyumbani kwa Madee. Anatakiwa aongee dhahiri asifiche, aongee tu ukweli.” Babu Tale ameeleza.
Amegusia pia tukio ambalo lilimsikitisha zaidi wakati Dogo Janja anafanya kazi akiwa chini ya menejimenti ya Mtanashati Entertainment.
“Siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga, wakati yuko South Africa alipost picha ‘ningekuwa Tip Top nisingefika huku’. Nilishangaa heeh huyu kutoka huko kijijini kwao alifanyaje hadi kufika hapa!