Blogger Widgets

March 8, 2014

Tazama Picha za Binti aliyekuwa kwenye imana ya Freemasons na aliwekwa ndani ya bahari kwa miaka mingi huku kidole chake kikiwa kimekatwa


Aliyekuwa Freemason kwa miaka 14 afunguliwa katika mkutano wa Ufufuo na Uzima unaoendelea Moshi; alikatwa kidole akiwa mdogo kama udhihirisho wa alama yao (devil horns)

alieleza mwenyewe mbele ya waliokuwepo mkutanoni maelfu ya watu wa mkoa wa Kilimanjaro na vitongoji vyake wanaohudhuria mkutano huo katika viwanja vya mashujaa unaoongozwa na mchungaji Josephat Gwajima wa kanisa la Ufufuo na Uzima lenye makao makuu yake Kawe jijini Dar es salaam.

Binti wa kiislamu ambaye aliwekwa ndani ya bahari kwa miaka mingi; alipokea ukombozi wake mara baada ya maombezi. Kule baharini alikuwa ameolewa na jini ambaye alimweka awe malkia wa baharini kwa miaka mingi... Mungu akamrudisha baada ya maombezi na kumpokea Yesu Kristo.

Baadhi ya picha jinsi maelfu ya wakazi wa mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro wanavyohudhuria mkutano huo toka ulipoanza tarehe 20 mwezi huu, unatarajiwa kumalizika siku ya jumapili tarehe 27.

Njia ni moja tu nayo ni YESU, askofu Gwajima akifundisha mkutanoni.




No comments:

Post a Comment