Blogger Widgets

March 16, 2014

Tazama Picha za Majabu ya Huyu mwanamke Mtalaka ambaye ni Raia wa Uingereza Amanda Rodgers aliyefunga Ndoa na mbwa Baada ya Kukosa Mume anayemfaa kwa Muda Mrefu


Mtalaka ambaye ni Raia wa Uingereza  Amanda Rodgers ametoa kali ya mwaka baada ya Kufunga Ndoa na Mbwa wake kipenzi aliyempa Jina la Sheba baada ya kudai kuwa na mapenzi ya dhati na Mbwa wake huyo kwa muda mrefu sasa.

  Amanda Rodgers ameolewa na Mbwa wake huyo (Sheba ) katika harusi iliyofana kwa namna ya kipekee huko Nchini Croatia katika hafla iliyohudhuriwa na watu takribanni 200.

Mtalaka huyo wa miaka 46 aliyekuwa amevalia kigauni chenye rangi nyeusi huku bwana harusi ambaye ni mbwa akiwa amevalia Shela Jeupe. Wapendanao hao walionekana kuwa na Nyuso za furaha huku Amanda Rodgers Akisisitiza kuwa Aliamua kufanya Uamuzi huo baada ya Kutengana na mumewe wa Ndoa miaka 20 iliyopita.
Amanda Rodgers Akiwa na Mumewe Sheba
 “Mbwa huyu(Sheba) Nimekuwa nae Maishani kwa kipindi kirefu sana, yeye ndiye ambaye ananifanya nicheke, nifurahi na kunituliza pindi ninapojisikia vibaya”