Blogger Widgets

April 21, 2014

Kajala Afunguka Mazito Juu ya Wema Sepetu Huku akitoa Machozi

Staa wa Bongo Muvi, Kajala Msanja katika pozi.
Maisha yanabadilika kwa spidi ya ajabu ndiyo maana ukweli wa leo unaweza kuwa uongo wa kesho!

Kwa kitambo kirefu mastaa wawili wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja na Wema Isaac Sepetu walikuwa kama kumbikumbi. Marafiki wa kufa na kuzikana. Sasa mambo yamebadilika.
Walizoea kulala hadi kitanda kimoja. Walikula na kunywa, walifanya kazi pamoja. Jioni walikwenda kujirusha pamoja.


Kajala Masanja na Wema Sepetu.
KAMBI ZAIBUKA
Wiki kadhaa zilizopita upepo ulibadilika. Kukawa na kambi mbili. Kila moja ikichafua upande mwingine. Anayeumizwa zaidi ni Kajala ambaye chanzo cha yote ni Sh. Milioni 13 alizolipiwa na Wema alipohukumiwa kifungo cha miaka 7 jela au kulipa kiasi hicho cha fedha kama faini.
 

Hoja ya kundi linalojiita Team Wema ni kwamba Kajala anamuonesha Wema dharau huku akitoka kimapenzi na yule kigogo wa Wema aitwaye Clement au CK ili kumchoresha mwanadada huyo (wanamwita Madam). Ili kukata mzizi wa fitina, tunakuletea exclusive interview na Kajala ambaye anafunguka mambo yote yaliyotokea.

UNGANA NAYE...
Wikienda: Kwa nini umegombana na Wema?
Kajala: Sijagombana naye, labda yeye tu.
Wikienda: Inasemekana huzungumzi naye na tayari ana mashosti wengine kama kina Aunt Ezekiel na Snura Mushi. Je, ni kweli?

Kajala: Nilichati na Wema kama siku tano hivi zilizopita. Kuhusu marafiki, Wema ana marafiki wengine wengi siyo mimi tu. Hata wakati nikiwa naye alikuwa nao.
Wikienda: Umesema uliwasiliana na Wema kupitia mtandao tena kama siku tano hivi zilizopita. Kwa watu marafiki wa kufa na kuzikana huoni kama ni tatizo?
Kajala: Sielewi chochote!

Wikienda: Wewe na Wema mnagombea nini hasa?
Kajala: Mimi nashangaa ghafla tu kundi la watu linanitukana mitandaoni. Hata Wema mwenyewe hawajui. Ishu ya milioni 13 ndiyo imekuwa habari ya mjini.
 

Natukanwa sana. Mwanangu anashindwa kusoma, anajifungia ndani na kulia siku nzima kwa kusikia mama yake akiitwa malaya (maskini analia).

Unajua mwanangu amekua, anaambiwa na kuona ninavyotukanwa hivyo lazima ajisikie vibaya. Mwanangu anateseka, anafanya vibaya darasani (yupo darasa la saba). 

ANATAKA KURUDISHA MIL. 13?
Wikienda: Kuna taarifa kuwa unataka kuzirejesha hizo Sh. milioni 13. Inasemekana upo tayari kuuza gari lako jipya (Toyota Bravis). Kajala: Nitazirejesha vipi wakati alinilipia hakunikopesha? Sijui kama inawezekana. Sijauza wala sina mpango wa kuuza gari ili nikamlipe hizo Sh. milioni 13.
 

TATIZO LILIANZAJE?
Wikienda: Tatizo lilianzaje?
Kajala: Nakumbuka maneno yalianza baada ya kwenda kufanya shoo Arusha. Tuliporudi mwenzangu akaanza kubadilika. Baada ya Arusha tulikutana tena saluni maeneo ya Kinondoni (Dar). 


Nilifika pale na baiskeli, nilitokea location. Nilikuwa na majasho sana si unajua kuendesha baiskeli?

Kumbe yeye (Wema) alikuwa ghorofani kwenye ile saluni.
Mimi nilikaa ili nipigwe na upepo au kiyoyozi ili nikae sawa.

Aliposhuka akaniona, alitaka kunikumbatia. Nikamwambia nooo...nina jasho, akamaindi ileile na ku-shout (kelele) eti mimi nimekataa kumkumbatia. 

KAMCHUKUA CLEMENT?
Wikienda: Inasemekana wewe umemchukulia aliyekuwa bwana’ke Clement aliyeachana naye, wewe ukaona umchoreshe hivyo akamaindi, hilo likoje?


Kajala: Katika maisha yangu niliwahi kuonana na Clement mara moja tu. Sina hata namba yake ya simu, sasa sijui nimemchukuliaje! 

USAGAJI
Wikienda: Inadaiwa wakati mkiwa na urafiki, mlikuwa mnashiriki mapenzi ya jinsia moja (usagaji). Je, ni kweli?

Kajala: Ni kweli nikuwa nalala naye kitanda kimoja, sasa hapo kwenye usagaji nani ‘mwanaume’ na nani mwanamke?
Wikienda: Inasemekana wewe ndiye ulikuwa ‘mwanaume’!
Kajala: Huuh...hakuna kitu kama hicho.
 

ANAMCHUKIA DIAMOND?
Wikienda: Madai mengine yanasema umekorofishana na Wema kwa sababu karudiana na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mara nyingi wanakuwa wote chumbani hivyo unakosa nafasi ya kujiachia naye. Je, ni kweli unamchukia Diamond?

Kajala: Kwa nini nimchukie Diamond? Sina shida naye. Huwezi kumchukia binadamu mwenzako hata kama kuna sababu.