Blogger Widgets

April 27, 2014

Muendelezo wa Matukio ya Ray na Chuchu Hans

KUKOPI na kupesti bila kuboresha! Mastaa wenye mapenzi kama ya njiwa kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ wamekuwa wakitupia swaga za picha kama zile za Kim Kardashian na mwandani wake, Kanye West.
Wasanii wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans na Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ wakijiachia.
Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Chuchu na Ray ambao majina yao yameunganishwa na kuwa Chura wamekuwa wakichukua sampo za picha za akina Kim nao kujifotoa kisha kuzisambaza.
“He! Mmewaona Chuchu na Ray? Eti wanakopi na kupesti swaga kama zile za Kim na Kanye kisa mapenzi yamekolea,” alisema mdau mmoja baada ya kuziona picha hizo mtandaoni

No comments:

Post a Comment