Blogger Widgets

April 5, 2014

Soma Ukweli Juu ya Ukweli ya Uhusianao wa Kimapenzi ya Salama Jabir na Mzungu Kichaa

Msanii wa Denmark aliyeishi Tanzania muda mrefu, maarufu kama Mzungu Kichaa amezungumzia uvumi uliowahi kusambaa kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mtangazaji wa kipindi cha ‘Mkasi’, Salama Jabir.
mzungu kichaa
Mzungu Kichaa amekanusha uvumi huo na kusema hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Salama.
“Sio kweli mimi si-date na Salama Jabir” Alisema alipohojiwa na katika kipindi cha TV cha Sporah, “tulifanya kazi pamoja kama majaji katika kipindi cha TV (BSS), so kuna vitu vingi ambavyo tunafanana pia alisoma UK na ni mtu mzuri, so ni marafiki tu kulikuwa na uvumi ulisambaa kwenye media”.
Salama

Salama Jabir

Pamoja na kuwa hakuna ukweli wowote juu ya swala hilo lakini Mzungu Kichaa amedai kuwa kuna mtu aliwahi kumuuliza kama ana uhusiano na Salama na alimjibu ndio lakini hakumaanisha.
mzungu na sporah
Mzungu Kichaa katika Sporah show

“kuna mtu aliniuliza nikiwa uwanja wa ndege, Mzungu Kichaa ni kweli una uhusiano nae, ilinibidi niseme ndio kwasababu nilikuwa nacheka sababu ilikuwa ni idea ya kuchekesha kwamba Mzungu Kichaa ana uhusiano na Salama.” Alisema Mzungu Kichaa.
Akiuzungumzia uhusiano wake na Salama amesema,
“Sisi sio best friends so sio kwamba tunatoka sana pamoja, ninayo namba yake, na yeye lazima atakuwa nayo ya kwangu lakini hatutumiani ujumbe kila wakati.”
Katika hali ya utani mzungu Kichaa alisema:
“People thought it was really funny and they got excited about it because imagine if these two, the crazy white man and the crazy Salama, coz Salama is crazy imagine if those two have children how crazy they will be.”

Aliongeza kuwa baada ya kusikia kinachozungumzwa mitaani aliwasiliana na Salama kumjulisha,
“Nilimtumia barua pepe kumwambia kile kinachosemwa na watu ili asije kushtuka akija kusikia”.