Blogger Widgets

April 14, 2014

Tazama Jinsi Uandaaji wa Video ya Weusi Gere Inavyofanyika huko Kenya

Zile teaser za Weusi zilizokuwa na title ya ‘OTEA’ ambazo wamekuwa wakiziweka kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii kuanzia wiki iliyopita, tayari imefahamika kuwa ni ujio wa video ya single yao mpya ‘Gere.
weusi gere
Nikki wa Pili wa Weusi ameiambia Bongo5 kuwa wameshoot video ya ‘Gere’ Nairobi ,Kenya siku chache zilizopita na director Enos Olik aliyefanya video ya Jaguar ‘Kioo’.
Gere video3
moja ya screen shots za ‘Gere’
Hapo awali ilikuwa inafahamika kuwa kulikuwa na mpango wa video hiyo kufanywa na Nisher, lakini Nikki ameelezea sababu za mabadiliko yaliyojitokeza mpaka kuamua kufanya na Mkenya.
“Bahati mbaya Nisher alikuwa yuko caught up na mambo mengi na sisi tulikuwa na haraka so tukashindwa, kwasababu Arusha na Nairobi sio mbali tukavuka tu boda tu fasta.”
Kama wewe unawafollow Nikki Wa Pili, G-Nako au Joh Makini sina shaka umeshakutana na post kama hii:
‘Joh_makini :Otea(gere video) iko tayari kwa yoyote anayetaka xclusive ya siku tano ya video hii..wasiliana na weusi company….’ hii ni post ya Joh Makini Instagram.
Gere video2

Weusi wamesema kabla video ya ‘Gere’ haijatoka wanataka kuifanyia biashara kwa yeyote anayetaka kuipata exclusive kwa siku tano kabla haijatoka rasmi iwe ni kampuni, blogs, au mtu binafsi.
“Hiyo ni biashara kwa mfano labda kampuni labda Voda au nani tunaweza tukawapa wakaweka kwenye page yao labda ya Facebook ikawa inapatikana pale tu”.
gere video1
Nikki ameongeza kuwa video ya ‘Gere’ itatoka wiki ijayo.
From:Bongo5

No comments:

Post a Comment