Blogger Widgets

April 5, 2014

Tazama Picha za Muimbaji wa kike wa Nigeria aliyedai ataitoa bikira yake kwa mwanaume atakayemnunulia mama yake ndege

Muimbaji wa kike wa Nigeria, Adokiye Kyrian amesema bado ni bikira na ataendelea kuwa hivyo hadi pale atakapopata mwanaume sahihi.
Singer-Adokiye
Kwenye mahojiano na jarida la Vanguard, muimbaji huyo mrembo alisema: Hujawahi kuona msichana mrembo ambaye ni bikira? Mtu yeyote atakayemnunulia mama yangu ndege binafsi nimemuahidi (mama yangu) ataushika moyo wangu.”
576885_505038269554965_690440405_n

Aliongeza kuwa haamini katika mapenzi na ana uhusiano na career yake tu. Amesema usanifu wa majengo (Architecture) ndiye mumewe muziki ndio boyfriend wake. Adokiye anaamini kuwa mapenzi ni hatari na kwamba hakuna mapenzi ya kweli. Akiwa na miaka 23 muimbaji huyo sasa ni balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa.