Blogger Widgets

April 21, 2014

Tazama Picha za Ndugu waliokamatwa kwa kesi ya Kula nyama za Maiti.wanandugu hao wanaotoka katika mji mdogo wa Darya Khan wamewahi kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kula nyama za binadamu. Waliachiwa huru baada ya kumaliza kutumikia adhabu hiyo mwaka jana.


Watu wawili wanaotuhumiwa kula nyama za binadamu wamekamatwa baada ya kichwa cha mtoto wa miaka mitatu, kukutwa katika nyumba wanayoishi nchini Pakistan.

Polisi waligundua tukio hilo la kutisha na kuwakamata watuhumiwa Mohammad Arif Ali (35) na mdogo wake Mohammad Farman Ali mwenye miaka 30.

Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Dailymail, wanandugu hao wanaotoka katika mji mdogo wa Darya Khan wamewahi kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kula nyama za binadamu. Waliachiwa huru baada ya kumaliza kutumikia adhabu hiyo mwaka jana.

Arif na Farman walikamatwa na kuswekwa rumande wakati uchunguzi ukiendelea, baada ya tukio hilo lililowavuta wengi na kutikisa tena eneo hilo.

Miaka mitatu iliyopita ndugu hao walifukua zaidi ya miili 100 ya maiti katika makaburi yaliyopo karibu na kijiji chao kisha kuzitumia maiti hizo kama asusa.

Mkuu wa Polisi katika eneo hilo, Ameer Abdullah alisema maofisa wake wa polisi waliamua kuvamia na kufanya upekuzi katika eneo hilo, baada ya majirani kulalamika kwamba kuna harufu mbaya ambayo imekuwa ikitoka katika nyumba waliyokuwa wakiishi.

“Wakazi hao waliifahamisha polisi baada ya kusikia harufu mbaya ikitokea katika nyumba waliyokuwa wakiishi watu hawa,” alisema Abdullah.

Abdullah alisema: “Tulifika katika nyumba hiyo siku ya Jumatatu asubuhi na kufanya upekuzi kabla ya kukiona kichwa cha mtoto wa miaka mitatu.

“Baada ya kugundua kitu hicho kinachotisha, tulimkamata mmoja wa ndugu hawa Mohammad Arif na alitupatia ushirikiano hadi tulipomweka kizuizini ndugu yake,” alisema Abdullah.

Alisema jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kung’amua iwapo kuna makaburi mengine yamechimbwa na watu hao kijijini hapo au katika vijiji vya jirani.

Baada ya kuulizwa maswali mengi na polisi, ndugu hao walikiri kula nyama za watu na kueleza ukweli namna walivyokuwa wakitengeneza mlo huo. Kwa kuwa Pakistan haina sheria zinazohusu ukatili wa maiti, huenda haitakuwa rahisi kwa wawili hao kufungwa jela maisha.