Blogger Widgets

May 3, 2014

Ukweli Juu ya Aunt Ezekiel Kuponda Mali za Mume wake wakati Mume wake Yupo Ndani

Habari za mjini zinadai kuwa, staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel yuko Dubai akiponda raha huku mumewe, Sunday Demonte akidaiwa kuwa jela jijini Abu Dhabi katika nchi za Falme za Kiarabu (UAE).
 
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiponda raha.
Awali, ilidaiwa kuwa, Aunt aliondoka  Bongo kwenda Dubai kuungana na mumewe katika ndoa, lakini vyanzo vya karibu vikahoji mumewe yupi? Mbona yuko jela baada ya kudakwa kwa kuishi kinyume cha sheria!
CHANZO CHATIRIRIKA
Kwa mujibu wa chanzo hicho, taarifa za mumewe kuwa jela,  Aunt alizichukulia poa kwani baada ya tu ya habari hizo Aunt aliendelea kujirusha katika kumbi tofauti jijini Dar na hata nje ya Dar kana kwamba hakuna kitu kilichotokea.

“Aunt hakushtuka chochote taarifa zilimfikia mapema, lakini hakuchukua hatua yoyote hata kule kuonesha kwamba amehudhunika,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Kama hamuamini tembeleeni katika kumbi za starehe kila siku tunakula naye bata kama kawaida, angekuwa mwingine angejaribu hata kuwa karibu na ndugu wa mume kushirikiana na kujua taarifa za mumewe.”
Staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel akiwa na mumewe Sunday.
AUNT ALIPOKEAJE MUMEWE KUFUNGWA?
Kumbukumbu zilizopo katika makrabasha ya Magazeti Pendwa zinaoonesha kuwa, Aunt alipoulizwa na mapaparazi wetu kuhusiana na taarifa hizo, alikiri kuzifahamu lakini akafafanua kuwa mumewe alikamatwa na kuachiwa huru lakini watu wa karibu wameendelea kupinga.

“Mume wangu amekamatwa ndiyo lakini si kama watu wanavyosambaza maneno wanayoyajua wao na kupindisha ukweli, alikamatwa kutokana na suala la kibali cha makazi kwisha muda wake lakini amesharekebisha, ameachiwa,” alisema Aunt.
HAONEKANI BONGO, DUBAI
Licha ya Aunt kudai mumewe huyo alikamatwa na kuachiwa, lakini tangu alipotamka kauli hiyo mwishoni mwa mwaka jana hadi sasa, mwanaume huyo hajawahi kuonekana hadharani.

 
“Tangu alipokamatwa hakutoka tena na ishu yenyewe aliyokamatwa nayo inasemekana ni mbaya hivyo si rahisi kutoka,” kilisema chanzo hicho bila
kufafanua ni ishu gani.

MAPAPARAZI WETU WAMNASA
Wakati taarifa hizo zikiendelea kusambaa jijini Dar, mapaparazi wetu waliwahi kumnasa staa huyo katika viwanja tofauti vya starehe kwenye miji ya Arusha na Dar es Salaam.

Uchunguzi wa mapaparazi wetu ulionesha kuwa kabla na baada ya taarifa za mumw kukamatwa kusambaa, Aunt hakuonesha tofauti, aliendelea kula kunywa na kucheza kama kawaida.
AUNT AENDELEZA BATA
Mapama wiki hii, Aunt ambaye yupo Dubai aliposti picha katika mtandao wake wa Instagram na kuonesha jinsi gani anakula raha huko.

 

Picha hizo zinamuonesha mrembo huyo akiwa katika bwawa maalumu la kuogelea (swimming pool) huku akinywa vinywaji tofauti hali ambayo ilileta tafsiri kwa mashabiki wake kwamba ni kuponda raha huku mumewe akidaiwa kuwa jela.
“Sasa huyu (Aunt) jamani vipi, badala apambane kujua hatima ya mumewe yeye yupo bize kula raha za mjini utadhani ana furaha,” alichangia shabiki
wake mtandaoni.

AWACHEFUA MASHEMEJI
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa mara baada ya kuzagaa kwa picha hizo katika mitandao ya kijamii, baadhi ya mashemeji wa Aunt walikuja juu na kudai wanamshangaa ni vipi haoni hali ilivyo na hawamsikii akizungumzia lolote kuhusu ndugu yao.

“Mashemeji zake wamekasirika kwelikweli kwani kuzagaa kwa picha hizo mtandaoni kunaleta tafsiri kwamba Aunt hana mpango na Demonte,” kilisema chanzo.
WIFI AZUNGUMZA
Katika kusaka data zaidi za ndugu wa Demonte, paparazi wetu alimtafuta mmoja wa mashemeji hao wa Aunt ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini ambapo alisema wamechukizwa na picha hizo na wanajipanga kumpa talaka.

“Huu si ubinadamu hata kidogo, sasa kwa kuwa ameamua kumwaga mboga sisi tutamwaga ugali, dawa yake tunamuandalia mipango ya talaka ambapo tukimpata Demonte kwa njia yoyote na akabariki talaka, tunampa muda wowote,” alisema shemeji huyo huku akikiri kuwa hata wao hawajui Demonte yukoje kwa sasa baada ya kupoteza mawasiliano naye.