Blogger Widgets

November 23, 2012

Dili lingine la Arsenal lililosainiwa na Emirates




Klabu ya soka ya Arsenal imetia saini ya makubaliano mapya ya pauni za kiingereza  £150m na kampuni ya usafirishaji ya anga ya  Emirates , na kuongeza udhamini wa wa kuvaa jezi zenye nembo  ya kampuni mpaka  2019. 

Vile vile matumizi ya jina la kiwanja cha   Emirates  Yaliyopo kaskazini mwa london pia yameongezwa mpaka   2028 ikiwa ni sehemu ya kandarasi hiyo  .

Kiujumla makubariano yataiingizia mil  £30m kwa msimu katika mauzo ya jezi na udhamini wa uwanja.


Mkataba huu mpya ni mkubwa  ukilinganishwa na wa vilabu vikubwa kama  Liverpool katika swala la mapato .

"Dili hii na kampuni ya  Emirates ilikuwa moja kati ya nafasi yetu kuhama katika uwanja wa zamani wa Highbury na katika hatua inayofuata mahusiano yetu yatakuwa maalumu kutuweka katika ushindani hapa uingerezana ulaya ," Amesema Mtendaji mkuu wa Arsenal  Ivan Gazidis.