Blogger Widgets

November 18, 2012

Kijitonyama::Mke wa mtu afumwa akivunja amri ya sita na jamaa mmoja japokuwa ana mimba ya miezi nane wakati mume wake akiwa kaenda kulala msibani kigamboni






NI aibu iliyoje? Mke wa mtu ambaye ni mjamzito wa
 takribani miezi nane, amefumwa laivu akifanya uchafu na
 njemba ndani ya Bajaj...

Tukio hilo la kuhuzunisha kwa kiumbe alichokuwa nacho 
tumboni, lilinaswa na mapaparazi wetu pembeni mwa 
Barabara ya Kaijenge, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, usiku 
wa kuamkia Alhamisi wiki hii...

SAA 6:30 USIKU

Mapaparazi wetu, wakiwa kazini saa 6:25 usiku, katika hali 
isiyokuwa ya kawaida waliona Bajaj ikiwa imeegeshwa 
pembeni mwa barabara chini ya miti huku ikiwa na watu 
ndani.

Baada ya kuitilia shaka, waliifuata na walipoikaribia 
walishuhudia ikitikisika huku kukiwa na miguno ya watu 
waliokuwa wakivunja amri ya sita (kuzini).

WAKURUPUSHWA

Walipoifikia Bajaj hiyo, waandishi wetu walipigwa na
 butwaa 
kumshuhudia mwanamke huyo akiwa na tumbo kubwa 
akifanya tendo hilo na njemba ambapo wawili hao 
walikurupuka na kuanza kutoka nduki huku wakiacha baadhi
 ya nguo.


Pamoja na kupigwa picha wakiwa ‘ovyo’, mwanaume 
alimshinda mwanamke kasi ya kukimbia hivyo kutokomea 
kusikojulikana lakini mwanamama huyo alishindwa 
 kutokana na ‘kuchoka’ kwa ujauzito.

MAHOJIANO

HOT POT lilimuweka ‘mtukati’ mwanamke huyo ambapo
 mahojiano yalikuwa hivi;

HOT POT: Mama jina lako nani, unaishi wapi na ulikuwa
 unafanya nini na huyo mwanaume kwenye Bajaj?

Mwanamke: Siwezi kuwatajia jina wala sehemu ninakoishi 
kwa sababu ninyi siyo polisi, kwanza mniambie ninyi ni nani 
ndiyo nitawajibu maswali yenu.

HOT POT: Sisi ni waandishi wa habari, kwa hiyo tunaamini 
utatujibu maswali yetu.

Mwanamke: (huku akilia kama mtu anayeomboleza msibani) 
Jamani naombeni mnisamehe, mimi ni mke wa mtu, 
nimeolewa, mume wangu amekwenda kulala msibani 
 Kigamboni (Dar), tumefiwa, mkiweka picha gazetini 
mtaniumbua…

HOT POT: Kwani mlikuwa mnafanya nini kwenye Bajaj na
 yule mwanaume ni nani?

Mwanamke: Sijui chochote, hapa nilipo
 nimeshachanganyikiwa.

Baada ya kushindwa kuzungumzia tukio hilo la aibu huku 
akiangua kilio, mwanamke huyo alisimamisha Bajaj nyingine 
iliyokuwa ikikatiza, akadandia na kutokomea kusikojulikana.

NI KAMCHEZO KALIKOZOELEKA

Hata hivyo, HOT POT hili lilizungumza na mlinzi anayelinda 
jirani na eneo hilo ambapo alithibitisha kuwa maeneo hayo 
yamekuwa na matukio mengi ya sampuli hiyo...