WESTERN CAPE, Afrika Kusini
POLISI katika mji wa Western Cape nchini Afrika kusini bado wanamuwinda mwanamke anayedaiwa kumgeuza bintiye mwenye umri wa miaka 13, kuwa mtumwa wa mapenzi kwa kumuuza kwa Randi 50 (shilingi 6000) na kutumia fedha anazozipata kunywea pombe.
Mwanamke huyom anadaiwa kuwa mara kwa mara alikuwa
akimchukua msichana huyo na kumpeleka vichakani au nje ya mji na
kumuuza kwa wanaume mbalimbali. H ata hivyo anadaiwa kuwa alikuwa mlevi
na mtumiaji wa madawa ya kulevya na kusababisha mtoto huyo kubakwa mara
kwa mara.
Madai ya unyanyasaji kuhusu mtoto huyo
yalijulikana baada ya mtoto huyo kumwambia mmoja wa marafiki zake,
ambaye aliamua kumweleza suala hilo mwalimu wao. Mtoto huyo kwa sasa
amehifadhiwa katika makazi ya wakimbizi ya Atlantis akipatiwa ushauri
nasaha na mshauri Barbara Rass.
"Ninampongeza mwalimu, kwani amevunjwa ukimya
uliokuwa umegubikwa. Ni kama kila mmoja sasa anajua nini kilichokuwa
kikiendelea, hakuna mtu ambaye angetambua kama kuna lolote linaendelea
kama yeye asingemweleza rafiki na kisha mwalimu kujua jambo hilo,"
alisema Rass.
Siku ya Jumatatu, kesi ilifunguliwa rasmi na
polisi ambao waliendelea kuchunguza madai hayo ya kesi ya ubakaji na
kumwingiza mtoto katika biashara ya ukahaba.
Rass mwenye umri wa miaka 35 ana uzoefu katika
kesi mbalimbali zinazofunguliwa na jamii na waathirika wa mashambulizi
na vitendo vya ngono, alikuwa akilia wakati akielezea kuhusu kesi hiyo
ya kutisha.
Alisema binti huyo alimweleza jinsi mama yake
alimpeleka katika madanguro mbalimbali ili afanye ngono na wanaume
wazee. Vitendo hivyo Rass anasema vilifanywa karibu kila siku usiku
wakati binti huyo aliporejea nyumbani akitokea shuleni.
"Mama yake alimchukua na kumpeleka katika
madanguro na kumwambia 'huyu ni mwanamume kwa ajili yako'. Au alimpa
chokleti na kumwambia 'En hier is vir jou 'n man [na huyu ni mwanamume
kwa ajili yako]'. Alikuwa akiondoka na kwenda msituni na mwanamume
wakati mama yake akiendelea kunywa pombe," alisema Barbara.
Wakati timu ya Dailyvoice ilipotembelea eneo
alilokuwa akiishi mwanamke huyo siku ya Jumanne, Mabinti watano wenye
umri sana na binti huyo walikuwa wakitembea sehemu hizo hatarishi pasipo
mwongozo wa wazazi. Maeneo hayo ambako malori makubwa hupaki, kulikuwa
kumezungukwa na vichaka pamoja na vibanda kadhaa mbavyo inasemekana
usiku hugeuzwa madanguro.
Hata hivyo kutokana na ulinzi mkali uliowekwa eneo
hilo, mabinti hao waliishia katika mikono ya polisi wiki iliyopita.
Lakini muathirika anasema kuwa yeye alikuwa akiambiwa kuwa asiseme neno
lolote kwa mtu mpaka alipofika katika mikono ya Rass na kueleza ukweli
wa mambo.
"Licha ya kufika mikono salama bado binti huyo
hakutaka kutaja majina ya wanaume waliombaka na kusema kwamba mwanamume
wa mwisho kumbaka alikuwa wa kabila la Xhosa. Bado hakutaka kutaja
mahali anapoishi wala kuzungumza lolote, kisha akanambia tu baada ya
hapo nini kiliendelea" mshauri huyo anaeleza.
Licha ya ukimya uliokuwa umemwandama msichana
huyo, hatimaye Jumatano alizungumza namna alivyoteseka katika
unyanyasaji aliofanyiwa na mama yake. Alieleza namna alivyofanyiwa
ukatili wa kutisha na kuvumilia siku zote.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kimataifa
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kimataifa