Ni moja ya Kifaa pekee kilichokuwepo eneo hilo Trekta, likifukua kifusi ili kuokoa watu wanaodaiwa kufukiwa na kifusi hicho.
Baadhi ya watu waliwahi kufika kujaribu kutoa msaada bila mafanikio hapa wakiwa wamekwama baada ya kukosa vifaa vya kutosha.
Wahindi nao walikuwapo kutoa msaada hapa wakilielekeza Trekta kusogea mahala walipo wao wakihisi kuwa kuna mtu mahala hapo.
Waokoaji wakijitahidi kutumia mikono kuondoa kifusi hicho ili kuweza kuwaokoa watu waliofukiwa.
Trekta likiendelea kuondoa kifusi hicho.
Juhudi zinaelekea kulala.........
Moja kati ya magari yaliyokuwa eneo hilo likiwa limeangukiwa na mabaki ya jengo hilo.
Trekta likiendelea kuondosha kifusi......../
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, akihojiwa na wanahabari kuhusu tukio hilo.
Moja ya ghorofa lililo karibu kabisa na jengo hilo lililoanguka nalo likiendelea kujenga nalo pia likiwa na ghorofa 14.....
Sehemu ya wananchi wakishuhudia tukio hilo.
Vijana wakishusha mitungi ya gesi ili kuwasaidia kukata nondo.... baada ya kuona vimekosekana vifaa vya haraka.
Changamoto ya uokoaji ni ngumu, lakini vikosi
mbalimbali vinaendelea na zoezi hilo, ili kunusuru maisha ya waliofukiwa na
kifusi.
Hizi nia aina ya nondo ambazo kimsingi sio
imara kuweza kuhimili ujenzi wa ghorofa ndefu kama hili, kuna haja mamlaka
husika likatupia macho kampuni za ujenzi ili kuokoa maisha ya wajenzi na
watumiaji wa majengo hayo.
Askari wakiimarisha ulinzi wakati zoezi la
uokoaji likiendelea.
Jitihada za
kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali
miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
Jitihada za
kuwaokoa watu zikiendelea.
Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
Waokoaji.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi
(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam (CP), Suleima Kova kuhusu jengo la ghorofa 16 lililoanguka majira ya saa
mbili asubuhi katika makutano ya mtaa wa Indira Ghandi na Barabara ya Morogoro
jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha
Minangi. Katika ajali hiyo watu wawili wamekufa papo hapo. (Picha zote na Habari
Mseto Blog)
Waokoaji wakiwa kazini.
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova.
Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum (CP), Suleima Kova akiwa katika eneo la tukio. Kulia ni
Mbunge wa viti maalum (NCCR-Mageuzi James Mbatia.
Mabaki
ya jengo hilo lililoporomoka jijini da es salaam amablo lipo barabara
ya morogoro mtaa wa indiana.Huku ni mashuhuda watukio hilo wakiwa eneo
hilo muda huu..Maiti zaidi zinaokolewa bado idadi kamili haijafahamika
mpaka sasa.Endelea kupitia audifacejackson blogspot kwa taarifa ziadi