Blogger Widgets

July 10, 2012

HII NDIO SIMU ANAYOUZA JOSE CHAMELEONE WA UGANDA, ZIJUE BIASHARA ZAKE NYINGINE.


Millard Ayo na Jose Chameleone
Huu ni mwaka wake wa 12 toka ameanza kuwa maarufu kwenye muziki, Jose Chameleone anaetajwa kuwa kwenye list ya wanamuziki watano matajiri wa muziki wa sasa Afrika Mashariki, leo amekubali macho yako yasome vitu atakavyovitaja vinavyompa pesa nyingi tofauti na muziki kwa sasa.
Hii ndio simu inaitwa CHEMELEONE ambayo inauzwa kwenye maduka mbalimbali Uganda, unaweza kuwaka line yoyote ya mtandao wa simu.
Amesema Moja kati ya ishu anazopiga ni “kununua nyumba na kuziuza, kukodisha, pia kununua mashamba na kuyauza huko Uganda, na kuna biashara nyingine nimeianza juzi juzi ya CHAMELEONE MOBILE, nilikwenda China na kuungana na kampuni moja ya  China wakatengeneza simu inaitwa CHAMELEONE, hiyo ni moja kati ya kazi zangu kubwa… watu wanazinunua sana nyumbani Uganda, ni handset ambayo unaweza kuweka line ya mtandao wowote”
Kwenye line ya mwisho ChameleonE kasema “hii ni kujaribu kufikiria nje ya box pamoja na kujaribu kufanya mipango uliyokua nayo kichwani, na bado naendelea baada ya hizo simu nataka kutengeneza vitu vingi zaidi.. nataka jamii yangu inikumbuke kwa nilichowafanyia”
Hayo ndio aliyoyasema Staa wa muziki Jose Chameleone wa Uganda nchi inayotajwa kuwa na wasanii wanaoongoza kwa kuwa na pesa nyingi kuliko nchi yeyote Afrika Mashariki.
Tayari mpaka sasa kuna baadhi ya mastaa ambao wamejaribu kupiga dealz nyingine mbali na muziki akiwemo Lady JayDee ambae anamiliki Mgahawa, Jua Cali wa Kenya alitangaza kuanza kutengeneza headphone kama za Beat by Dre, Profesa Jay nae alitangaza kwamba ndoto zake hazipo kwenye magari ya kifahari sasa hivi au anasa nyingine, anajipanga kwa ajili ya kuinvest kwenye ardhi for now.

No comments:

Post a Comment