Baba Diamond alifunguka hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mara baada ya mapaparazi wetu kutia timu nyumbani kwake Magomeni Kagera jijini Dar.
Mzazi huyo alisema kuwa, anasikitishwa kumuoana Diamond akijisahau kiasi cha kushindwa hata kwenda kwake kumjulia hali.
“Diamond amejisahau sana, umaarufu alionao unamfanya ashindwe hata kunijulia hali? Mimi ni baba yake, haiwezekani akakaa kimya bila ya kunikumbuka, tena miye siyo mtu wa kumuomba shilingi Sh.50,000 kisha akashindwa kunipa,” alilalama mzazi huyo.
Mzee Abdul alimtaka Diamond kujua kuwa ustaa una muda wake na kumtaka akumbuke jinsi alivyopigana kwa nguvu zote kumlea.
Mazazi huyo aliendelea kutiririka kuwa, anayo mifano hai ya mastaa wengi wa Bongo Fleva ambao walivuma lakini kwa sasa hawavumi tena, hivyo kumuonya mwanaye (Diamond) awe makini yasije kumkuta kama ya wenzake.
Nasibu Abdu 'Diamond'.
“Watanzania wanatakiwa kumuombea maana nimesikia ameanza kuandamwa na
mabalaa ya ajali na vitu vingine. Tumuombee Mungu amuepushe na awekeze
fedha zake kwenye miradi maana muziki hautabiriki,” alisema baba
Diamond.Jitihada za kumpata Diamond ili azungumzie kauli ya mzazi wake, hazikuzaa matunda kwani simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.