Katika haraati za kujitafutia utajiri, Njemba moja nchini Nigeria
imemuua na kumfukia mtoto wake wa miezi minne kwa kile kinachodaiwa
kujitafutia utajiri. Tukio hilo la kinyama limefanyika katika Mkesha wa
mwaka mpya mpya. Hata hivyo siku chache zilizofuata kioja cha njemba
hiyo kiligunduliwa na sasa yupo mikononi mwa vyombo vya dola.
