Blogger Widgets

March 25, 2013

Top 7 za Warembo wa Bongo wanaoshine wakiwa wamekata Nywele Zao

Hawa ni warembo 7 ambao wamezoeleka kwa muonekano wao wa kunyoa nywele na ambao kwa kufanya hivi hutoka bomba zaidi.
Irene Kiwia

n556875725_1082022_2930
Irene ni mrembo wa zamani wa Miss Tanzania na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya PR ya Frotline Porter Novelli na Rais wa NGO ya Tanzania Women of Achievement. Ni mama wa watoto wawili wa kiume Zion Thierry na Ethan Theodore.
Miriam Odemba
5
Miriam Odemba ni Miss Tanzania Earth 2008 na Miss Earth Air 2008 (mshindi wa pili). Pia aliwahi kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Mnet Face of Africa mwaka 1999 ambako aliingia fainali.Kwa sasa Odemba ni mama na mfanyabiashara pia.
Flaviana Matata
293868_284220835029936_72674900_n
Flaviana ni mshindi wa shindano la kwanza la Miss Universe Tanzania mwaka 2007 na kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Miss Universe ambako alikamata nafasi ya 6. Alishindana kwenye shindano hilo akiwa na kipara. Kwa sasa ni mwanamitindo wa kimataifa akitumiwa kwenye mambo mbalimbali ya fashion duniani.

Kajala Masanja
kajala_masanja3
Umaarufu wa Kajala nchini ulitokana na uhusiano wake wa miaka mingi na producer P-Funk Majani aliyezaa naye mtoto mmoja. Alijulikana zaidi alipojiingiza kwenye Bongo Movies ambapo kwa mara ya kwanza aliigiza na Steven Kanumba pamoja na staa wa Nollywood Ramsey Noah. Tangu mwaka jana amekuwa mahabusu na leo hii siku ya hukumu yake amekuwa huru baada ya kupata hukumu ya kwenda jela miaka mitano ama kulipa faini ya shilingi milioni 13. Wema Sepetu amemlipia faini hiyo.
Jacqueline Wolper
jackie-wolper-filamu-ya-kumuenzi-kanumba-0

Jacky Wolper alijaribu kufuata muonekano wa mrembo wa Marekani Amber Rose ambao ulimtoa pia.
Nakaaya Sumari
nakaaya_0108
Hitmaker huyu wa Mr President anafahamika kwa muonekano huu ambao ndio utambulisho wake. Muonekano ambao humtoa bomba.
Emmy Melau
emmy
Emmy Solomon Melau kutoka Arusha alikuwa mshindi wa Face of Tanzania 2007. Taji hilo lilimfungulia njia ya kwenda kuishi Pretoria nchini Afrika Kusini ambako aliendelea na mambo ya fashion.