Blogger Widgets

April 27, 2013

Mcheck Msanii wa Kenya Alieibuka na Kuanza Kulilia Bikla Yake Na Sababu Alizotoa

Mwanamuziki  aliyeitikisa vilivyo Kenya kabla ya kuokoka na kuachana na miziki wa kidunia, mwanadada Size 8 sasa ameanza kufunguka katika interview kwenye vituo mbali mbali vya redio na Tv kuhusiana na maisha mapya ya kidini.

Kati ya yote ambayo Size 8 amekuwa akiyaongelea, ni moja tu ambalo amekuwa akilitilia mkazo kwa kumaanisha kuwa linamsikitisha zaidi ni suala lake la kupoteza BIKRA, Size 8 amewaambia watu kuwa  "Najutia sana kupoteza bikra yangu. Ninaamini kuwa kijana anatakiwa kujilinda na kujizuia kufanya ngono katika ujana wake wote mpaka atakapo pata kibali toka kwa Mungu."
Pamoja na hayo yote Size 8 amewakata mate wanaume wote wakware (wapenda ngono) kuwa sasa hana tena nia ya kujiingiza katika mahusiano yoyote ya kimapenzi na badala yake anatafuta MTU MMOJA atakaye kuwa mwanaume wake wa maisha.
Inasemekana kuwa Size 8 alifanya maamuzi ya kuokoka baada ya kufanya  mapenzi na mwanaume ambaye baadae alimdanganya kuwa ameathirika na HIV, lakini yeye hajaliongea ilo katika interview zake.