Blogger Widgets

May 14, 2013

Juma Nature aungana na Lady Jay Dee

USIPITWE,SIR JUMA NATURE KIBLA "KIROBOTO"AUNGANA NA PRO.J SHOW YA LADY JDMSANII mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Kassimu 'Juma Nature' ameungana na msanii wa kike wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Lady Jaydee' katika uzinduzi wa albamu yake ya sita iitwayo 'Nothing But The Truth' itakayozinduliwa Juni 31 mwaka huu.


Wasanii wengine ambao  wameungana na msanii huyo ni pamoja na msanii nguli wa muziki wa Hip Hop Professa Jay, TID  na Grace Matata .


Akizungumza jijini Dar es Salaam, Gadner G. Habash ambaye ni  Meneja na Mume wa Mwanamuziki huyo alisema kuwa Juma Nature ni miongoni mwa wasanii ambao ameamua kuungana na Jidee kuwepo katika uzinduzi huo.


Alisema kuungana kwake kumeongeza nguvu katika uzinduzi huo ambao utakuwa ni wa aina yake.