Blogger Widgets

June 7, 2013

Asubuhi Tulizungumzia Huyu Demu wakizungu Anasadikiwa Kuwa Alikuwa Demu wa The Late Albert Mangwea so Check Picha Za Matukia Ya Kusikitisha Aliyoonesha

   
Mzungu huyo akiwa dada zake Albet kutoka kuliani ni Anna Keneth Mangweha,Magreth Keneth Mangweha na Neema Keneth Mangweha

  Marafiki wa marehemu Albet Mangweha wakiwa kwenye picha ya pamoja na Shemeji yao 


Untitled



MAJONZI na vilio vilitawala juzi katika zoezi la kuuaga mwili wa marehemu Albert Mangweha ‘Ngwea’ kwenye Viwanja vya Leaders lakini mmoja wa waliotia fora katika kuangua kilio alikuwa dada mmoja mzungu anayedaiwa kuwa alikuwa Mpenzi wa Ngwea aitwaye Misheily.


Mzungu huyo alionekana akilia kwa uchungu huku akitoa maneno yaliyoashiria kuwa ameumia sana kuondokewa na ‘mtu’ wake huyo ambaye huenda walikuwa na malengo mazuri ya baadaye.


Aidha, kilio alichokuwa akiporomosha binti huyo kiliwafanya watu waliokuwa karibu naye kumsikitikia na kuzidishiwa majonzi kwani ilifika wakati akaishiwa nguvu.


Mwandishi wetu alijaribu kumfuata na kumuomba kuzungumzia juu ya kifo cha Ngwea lakini alikataa na kusema asingeweza kufanya hivyo kufuatia majonzi aliyokuwanayo huku akionekana kutoamini kama jamaa yake huyo ametutoka

  Mcumba wa marehemu Albet Maangeha Bi, Michelle Looise Hancock raia wa Uingereza akiweka shada la maua kwenye kaburi la mpendwa mchumba wake. jana

No comments:

Post a Comment