Blogger Widgets

June 13, 2013

Soma Maneno ya Baba Mzazi wa Marehemu Langa Baada ya Kifo Chake


Baba wa marehemu Mzee Kileo amesema kuwa mtoto wake Langa kwenye picha amefariki dunia leo majira ya saa 10 katika hospitali ya Taifa Muhimbili.Taarifa kamili na mipango ya mazishi zitatolewa pale vikao vya familia vitakapofanywa.Pia baba yake alisema msiba huu umetokea wakati mama yake Langa hayupo Tanzania,alisema kwa sasa mama yake Langa yupo Marekani lakini baada ya kupewa taarifa hizo tayari ameshakata tiketi ya kurudi Tanzania na ataanza safari kesho.Msiba uko nyumbani kwao maeneo ya Mikocheni