Blogger Widgets

July 8, 2013

Picha 60 zikionesha Jinsi Msanii Shilole na Masanja Mkandamizaji walivyojumuika Na Viongozi Mbalimbali Huko Marekani

Dj Luke akiambatana na mgeni wake Mhe. Ali Hassan Mwinyi kuelekea ukumbini kulikofanyika Tamasha la Utamaduni wa kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo Jumamosi July 6, 2013 na kuwa tamasha la kihistoria lililohudhuriwa na Watanzania wakiwemo wadau wanaozungumuza Kiswahili wapatao 600 kutoka kila kona hapa Marekani, Ulaya na Tanzania.
Kutoka kushoto ni Dj Luke, Mhe, Ali Hassan Mwinyi, Mhe. Ramadhan Muombwa Mwinyi, Mama Lily Munanka, Idd Sandaly na Baraka Daudi katika picha ya pamoja wakati wakiingia ukumbini.
Watoto wa darasa la Kiswahili DMV wakiimba wimbo wa Taifa.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi akiongea machache kabla ya kumkaribisha Dj Luke.
Dj Luke akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mama Lily Munanka.
Kaimu Balozi Mama Lily Munanka akishukuru kamati ya maandalizi na kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akihutubia mamia ya Watanzania waliofika kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na kulifungua rasmi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania New York, Bwn. Haji akisoma shairi alilotunga maalum kwa ajili ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la Utamaduni wa kiswahili Marekani.
Shilole na Masanja mkandamizaji wakikandamiza na kugaragaza kwenye Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na miaka 3 ya sherehe ya Vijimambo.
Shilole(mwenye gauni la punda milia) akimnyanyua Afisa Ubalozi Mindi Kasiga kwenye moja ya nyimbo zake alizotumbuiza kwenye tamasha hilo.
Mhe. Ali Hassan Mwnyi akiaga na kuelekea kwenye gari lililomleta tayari kwa kuondoka baada ya kumaliza sehemu ya kwanza ya tamasha hilo na sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo.
Mhe. Ali Hassan Mwinyi akiwa tayari kuondoka.
kwa picha zaidi bofya read more.





No comments:

Post a Comment