CharlieSilverwood_kolukirilancocuk_b
Mtoto mwenye umri wa miaka 11 shabiki wa mchezo wa soka nchini Uingereza amevunjika kiwiko cha mkono baada ya kupigwa na mpira wa ‘free kick’ iliyopigwa na nyota wa mpira wa miguu Cristiano Ronaldo.
Mtoto huyo Charlie Silverwood alibaki akijiinamia kwa maumivu baada ya mpira huo uliopiwa umbali wa yadi 35 kuvunja mfupa wa kiwiko cha mkoni mara mbili.
Hata hivyo kijana huyo alikuwa amedhamiria kutokosa kumalizia kuona mwisho wa mechi hiyo ya kirafiki kati ya timu yake ya Bournemouth na Real Madrid hivyo alibaki uwanjani kushuhudia dakika 84 za mchezo zilzokuwa zimebakia.
358054-Ronaldo-Shot-Breaks-Child-Wrist
Baada ya kumalizika mechi hiyo alipelekwa hospitali ambako mashine ya ‘X-rays’ ilionyesha kupasuka mara mbili.
Silverwood alisema hii ni moja ya namna za kipekee mtu unaweza kuvunjika mkono.
Akaongeza kuwa huwezi kutegeme tukio kama hilo kumtokea mtu na nisinge nyanyua mkono wangu wa kushoto, ningeishia kupoteza meno ya mbele.
Katika mechi hiyo Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 alifunga mabao mawili wakati wakali hao wa Hispania walipoilabua Bournemouth bao 6-0.
Real Madrid imemtumia mtoto huyo jezi iliyosainiwa na wachezaji kupitia mkongwe wa klabu hiyo ya Bournemouth steve Fletcher kama kumpa pole.
Pia mtoto Charlie amepewa mpira uliosainiwa na timu yake ya Bournemouth