Blogger Widgets

August 25, 2013

Check Diss Alizozipata Masanja Baada ya Kuweka Hii Picha Akiwa Jukwaani kama Mchungaji na Kuuombea Mtu aliyeanguka Kwa Mapepo


1235050_461227907309312_1001732574_n
  Safari ya kuelekea kuwa mchungaji na mhubiri mkubwa wa kikristo nchini kwa mchekeshaji wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya aka Masanja Mkandamizaji inaonekana kuwa ya milima na mabonde lakini haoneshi dalili za kurudi nyuma.

Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya akimuombea mgonjwa
Leo Jumapili kupitia ukurasa wake wa Facebook, ameweka picha inayomuonesha akiwa mbele ya maelfu ya waumini alipokuwa akihubiri neon la Mungu huku akimuombea mgonjwa aliyekuwa ameanguka chini.
“Nimeona Mungu wangu akiponya wagonjwa na kufungua walifungwa na magonjwa sugu. Ni maombi yangu Jumapili ya leo, kila jambo lililokusumbua kwa mda mrefu,iwe ni ugonjwa,shida ya Ndoa,kazI,biashara,masomo,laana,nk,Mungu wangu akuhurumie na upokee uponyaji. Tamka maneno haya kwa imani rafiki yangu, asante Mungu kwa kunihurumia,nimeponywa,” aliandika.
Hata hivyo mashabiki wake wamemshambulia huku wengine wakimweka kwenye kundi na manabii wa uongo.Haya ni baadhi ya maoni:
Swaleh InaSal
Hii yote alishasema mwenyewe kuwa watakuja manabii wa uongo na kujifanya wanaponya kama alivyokua akifanya yeye.. katu hamtaweza na kama ingekua kweli basi cha kwanza dunia ukimwi usingekuwepo acheni sanaa nyinyi msipotoshe watu.

William Kaizer

Masanja nae kawa mchungaji ahahahahahaaa


Chelsea Nsiko Ichanchu

Wanatumia uchawi kutuchukulia vijisenti vyetu;, kama kweli wanaponya watu waende basi mhimbili kuna wagonjwa wengi sana…..
Haroun M Mussa
Kamponye vengu kwanza kam sio ubabaishaji, punguzeni njaa
Deogratius Manyahi
Ila kiukweli wa kutoka rohoni! Huo umati 90% wamekuja kumshangaa Masanja na c kwa maombi. Maana wanamwonaga tu kwenye Tv. Na sasahv ha2na ving’amuzi ndo kabisaaaa.
July Macgwire
Hii mijitu bwana sijui hayana ubongo!!, Hawa wote wanaojita wachungaji mara manabii na mitume!! Ni matapeli….MATAPELI!!!!. Sasa ona huyo mnyalu anavyojidhalilisha kisa anataka kuwa na miliki zake…p****
Godwin Katemi Majahasi
Nina hakika Masanja Amri 10 Mungu hazijui na hazishiki, kwani ukimwangalia katika ze COMEDY Show anavunja sana AMRI YA PILI YA MUNGU ; USILITAJE BURE JINA LA BWANA MUNGU WAKO
Melkiadi Edward
Dini 2meletewa,ww ni nani kilaunae mwombea anapona?acheni kuwapotosha watu mwenye uwezo wa kuponyesha ni mwenyezi mungu tu,imani yako haifkii hata punje ya yorodani leo hii unaponyesha?mwenyezi akusamehe.
Hivi ndivyo mtumishi huyo wa Mungu alivyowajibu wale wasiomuamini:
Nina hakika nyote mnao comment ni rafiki zangu, bas someni vizuri status, Mungu ndiye atakaye waponya na kuwasaidia sio Masanja pls, hata rafiki zangu waislam mnamwamini Mungu na kumuomba pia, kuna watu mpaka mnaandika maneno mabaya kwani ni ugomviiiiiii.? Kwani kuna ubaya kumuomba Mungu juu ya rafiki zako, na kama huamini usi comment hapa kuna roho za watu Mungu anaziponya asubuhi hii hivyo wewe usitumike kuwakosesha wanaoamini kisa huamini. Bado nina msihi Mungu akubariki na kukuepusha na kila baya rafiki yangu. barikiwaaaaaaaaaaaaaaa. Marko 16:16 watakao amini wataokoka,wasioamini watahukumiwa, uzuri wake ilishajulikana kuwa hakukosi watu wasioamini. Sasa ni bora kutoamini na kunyamaza kuliko kutoamini na kujifanya mjuaji na unajua kuupinga uwezo wa Mungu.
From:Bongo5