Uwazi lilifanikiwa kunasa majina ya vigogo waliokamatwa wakiwa na unga na kiasi walichokamatwa nacho.
VIGOGO
111 wanaosadikiwa kujihusisha na biashara yharamu ya madawa ya kulevya
nchini wameanza kuonja 'joto ya jiwe' kufuatia Jeshi la Polisi Tanzania
Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya kwa kushirikiana
na vyombo vingine vya dola kukamata mali zao, Uwazi lina mpango mzima.
Kwa
mujibu wa vyanzo makini ndani ya jeshi hilo, pia vigogo wengi
wanaojihusisha na biashara hiyo walikamatwa na kiasi kikubwa cha ‘unga’
ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita.
Kuhusu
mali ambazo ni magari, ilidaiwa kuwa kufuatia taarifa zilizowataja wauza
unga, jeshi la polisi liliamua kushikilia magari hayo na kufanya
uchunguzi wa uhalali wake.“Kuna
watu walitajwa majina, wakafuatiliwa, magari yao yakakamatwa na
kufanyiwa uchunguzi, lakini cha kushangaza baadhi yao wameingia mitini
na kutelekeza magari yao,” kilisema chanzo.
Chanzo
kilisema baadhi ya magari hayo ni Mercedes Benz, Jeep, Toyota Spacio,
Toyota Galsira, Toyota Mark II, Nissan Patrol 4x4 GL, Toyota Land
Cruiser na Toyota Prado.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti hili katika mahakama mbalimbali nchini na ndani ya
jeshi la polisi umebaini kuwa, kesi za watuhumiwa hao zinaendelea
kuunguruma kortini japokuwa kasi yake si ya kuridhisha.Na Global
publisher
POLISI WABUNI MBINU MPYA
Vyanzo
hivyo viliendelea kudai kwamba polisi wamebuni mbinu mpya ya kuwakamata
vigogo wa madawa ya kulevya wakiamini itawapa mafanikio zaidi.
“Siku
hizi si kama zamani, jeshi la polisi tumebuni mbinu mpya ya kuwakamata
hawa jamaa (vigogo). Mbinu hii italeta mafanikio makubwa zaidi,” alisema
mtoa habari wetu.
WAPAMBANAJI WA UNGA HATARINI
Taarifa
zaidi zinadai kwamba usalama wa viongozi wanaopambana na wahusika wa
unga nchini upo shakani kutokana na vitisho vinavyotolewa na mtandao huo
duniani kote.
Inaaminika
kuwa wengi wanaopambana au kupiga vita madawa ya kulevya, hususan
viongozi na waandishi wa habari, hutendwa vibaya wakati mwingine kuuawa
kabisa.
UWAZI LAMSAKA KAMANDA NZOWA
Kufuatia
taarifa hizo za kiuchunguzi, katikati ya wiki iliyopita, mapaparazi wetu
walimtafuta Kamanda wa Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya
Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu zoezi zima la kamatakamata
ya wanamtandao hao.
Kamanda Nzowa alisema zoezi la kuwakamata wanaojihusisha na biashara hiyo linaendelea vizuri.
Alisema
mpaka Mei, mwaka huu kikosi chake kimeshakamata kiasi kikubwa cha unga
na kuongeza kuwa anaamini kasi ya biashara hiyo nchini imepungua sana.
Aliongeza kuwa askari wake wamejipanga vizuri na wana mafunzo maalum ya kuwatambua watu hao hatari.
VIGOGO HUWALISHA KIAPO KIBAYA WANAOWABEBESHA
“Tumewakamata ‘mapapa’ (wauza unga wadogo) wengi sana na tunahakikisha kwamba ‘nyangumi’ (wauza unga vigogo) nao hawachomoki.
“Mara
nyingi vigogo wamekuwa wakiwalisha kiapo kibaya vijana wanaowabebesha
unga kwamba ikitokea wakakamatwa wasiwataje lakini nao tunawabana
kitaalam mpaka wanawataja, kwa sasa bado tunaendelea kuwadaka,” alisema
Kamanda Nzowa.
Kamanda
huyo aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lake dhidi
ya wauza madawa ili kutokomeza kabisa biashara hiyo.
ULINZI VIWANJA VYA NDEGE NCHINI SASA NI MOTO
Katika
maongezi yake, Afande Nzowa alisema ulinzi umeimarishwa katika viwanja
vya ndege, bandarini, mipaka ya nchi na sehemu zote zinazohisiwa kuweza
kupitishwa madawa hayo.
AANIKA MAJINA 111
Kamanda Nzowa alikwenda mbele zaidi kwa kuweka wazi takwimu ya ukamataji wa watuhumiwa hao kutoka mwaka 2009 hadi Mei, 2013.
Orodha chini inabainisha kiasi na aina ya madawa waliyokamatwa nayo katika mabano.
Steven
Gwaza, (heroin gramu 825.7), Rebecca Wairimu Mwangi (heroin gram 1,800),
Khatibu Bakari Khatibu, Khalid Salim Maunga, (cocaine gramu 1,007.4),
Dhoulkefly Awadh, (cocaine gramu 893.58), Abdallah Pashua Kipevu
(heroin gramu 31,000), Diaka Brama Kaba (heroin gramu 31,000), huyu
alikamatwa akiwa na Ndjane Abubakar, Sylivia Kaaya Namirembe, Farid
Kisuule, Robinson Dumba Teise na Ismail Mugabi.
Wengine
ni Rashid Salim Mohamed, (cocaine gramu 1,374.32), Mini Thabo Hamza
(cocaine gramu 1,595.74), Hamis Mohamed Mtou (cocaine gramu 850), Kwako
Sarfo, Mnigeria (cocaine gramu 1,1951.80), Mustapha Musa (cocaine gramu
286), alikuwa na Aman Saidfadhil Daruweshi na Afshin Jalal.
Kamanda
Nzowa akaendelea kuwaanika, Jack Vuyo, (heroin gramu 42,000) huyu
alikuwa na Anastazia Elizabeth Cloete. Simon Eugenio Fadu (cocaine
gramu 8,000), Assad Aziz, (heroin gramu 50,000), alikuwa na Isamil
Shebe Ismail, Rashid Salim na Majed Gholamghader.
Wengine
kwenye orodha hiyo ni, Anna Jamaniste Mboya, (cocaine gramu 1,140),
Fredy William Chonde (heroin gramu 175,000), Kambi Zuber, Abdul Ghan na
Shahbaz Malik, Livinus Malik (Wapakistani) (cocaine gramu 804.7),
Chukwudu Denis Okechukwu, Paulo Ekechukwu na Hycenth Stan (Wanigeria)
(cocaine gramu 81,000).
Aidha
wapo, Shoaib S.O. Mohammed, Fedro Alfredo Chongo, (cocaine gramu 1,530),
Kadiria Said Kimaro (heroin gramu 1,365.91), Abdallah Rajab Mwalimu
(cocaine gramu 716.5), Mwiteka Godfrey Mwandemele (cocaine gramu
1,112), Abbas Kondo Gede (cocaine gramu 1,112), Mwanaidi Ramadhan
Mfundo (cocaiane gramu 5,000), alikuwa na Sarah David Munuo, Antony
Karanja, Benny Ngare, Almasi Hamis Said, Yahya Haroun Ibrahim, Aisha
Said Kungwi, Rajab Juma Mzome na John William Mwakalasya.
Wengine
ni Ally Mirzai Pirbakhshi (cocaine gramu 97,000) alikuwa na Aziz Juma
Kizingiti, Said Mashaka Mrisho, Abdulahman Mtumwa na Hamidu Kitwana
Karimu.
Ramadhan
Athuman (heroin gramu 3,000) alikuwa na Rashid Mohammed, Ally Mohammed
Kichaa na Issa Abdulahman. Rashid Ally Mtopea (heroin gramu 12,000)
alikuwa na Idd Adam Mwaduga, Nurdin Adam. Maurine Amatus Lyumba, John
Adams Igwenma wa (Mnaijeria) ( cocaine gramu 830.19).
Upendo
Mohammed Cheusi, Abdallah Omar Salum (cannabis sativa gramu 1,000)
alikuwa na Cosmos Chukwumezie, Ifeanyi Malven Kalu Oko (Wanaijeria)
(heroin gramu 3,185.38), Allan Duller (cocaine gramu 3,882.92), Alberto
Mendes kutoka Ghana, (gramu 1,277.10 za heroin)
Wengine
ni Joseph Chukwumeka Nwabunwanne Minigeria, (gramu 1,245.96 za heroin)
Kwaku Safo Brobbey Mghana (gramu 13,781.78 za heroin), Princewill Ejike
Mnigeria (gramu 981.12 za heroin),Mary Mvula Mzambia (gramu 391.51 za
cocaine), Waziri Shaban Mizongi, (gramu 2,013 za heroin) akiwa na Santos
Joseph Mpondela, Kelvin Kelven Mwazeni.
Wengine
ni Emmanuela Adom, Mghana (gramu 9,838.1 za cocaine), Asha Omary
Ramadhan, (gramu 1.56), Mariam Mohammed Said, (gramu 9,857.54 za bangi)
akiwa na Abdullatif A. Fundikira
Aliendelea
kuwataja Marceline Koivogui, Mghana (gramu 1,073.82 za heroin), Edwin
Cheleh Swen Mliberia (gramu 1,509.35 za heroin), akiwa na Benjamin
Obioma Onuorah wa Nigeria, Sofia Seif Kingazi, (gramu 3,379.54 za
cocaine), Josephine Mumbi Waithera Mkenya (gramu 3,249.82 za cocaine),
Iddi Juma Mfaume,( gramu 563.25 za heroine), Amina Kassim Ramadhani,(
gramu 1,980.11 za heroine) na Vivian Edigin Mnigeria ( gramu 797.56 za
cocaine), Hadija Tambwe,( gramu 33,507.04 Za cannabis), Sasha Farhan
na Mnyeke Sativa, na Mychel Andriand Takahindangeng Muindonesia,( gramu
3,932.44 za cocaine).
Wengine
ni Kristina Biskavevskaja Mluthenia (gramu 4,000 za cocaine), Stephen
Basil Ojiofor Mnigeri (gramu 1,173 za cocaine), Judith Marko Kusekwa, (
gramu 1,793 za heroin), Khamis Said Bakari,( gramu 1,793 za heroin).
Kundi la
mwisho ni Tabia Omary au Neema Omary (gramu 994.97 za heroin), Masesa
au Habiba Andrew Joseph, ( gramu 1,037.9 za heroin).
Hivi karibuni Agness Gerald ‘Masogange’ na mwenzake walikamatwa Afrika Kusini wakiwa na kilo 150 za dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment