Blogger Widgets

October 10, 2013

Irine Uwoya na Johari Chali Huko Arusha

IMG-20131007-WA0023(1)

WASANII wa filamu nchini “Bongohood” kushoto Irene Uwoya, Johari anayeongea na simu na kulia Jackline Wolper wakiwa “Miles Stone bar” iliyopo eneo la Sakina maarufu kama Baa mpya ya jijini Arusha, mwanzoni mwa wiki hii, Wakazi wa Arusha hawakuonyesha kusisimkwa na ujio wao huku idadi ndogo ya wakazi wa jiji hili la kitalii wakionyesha kutambua ujio wao.

Habari za ndani zinadai kuwa wasanii hao ni mara ya pili kufika katika baa hiyo ambapo mara ya kwanza walionekana na matajiri wa mawe “tanzanite” waliopo jijini hapa, Siku ya juzi hali haikuwa nzuri sana kwao baada ya kuonekana wapweke wakiwa wamejikunyata kama watoto yatima.

Mdodosaji wetu alibainisha kuwa kwa muda wote walio kaa katika baa hiyo walionekana kama Simba walio mawindoni huku meza zao zikiwa nyeupe na kuwafukuza waudumu pale walipotaka kuja kuwasikiliza.

Hata hivyo watu walio jitokeza kwenda kuvuta raha katika baa hiyo waliendelea na shuguli zao bila kuonyesha kuvutwa na uwepo wa Mastaa hao wa kike hivyo kupelekea wanadada hao wa Bongohood kulazimika kujiondoa maeneo hayo mapema kuliko ilivyo tarajiwa.

IMG-20131007-WA0026

Juu picha ikionyesha namna warembo hao walivyokuwa wapweke huku wakijaribu kumuondoa muudumu wa baa hivyo yenye kuwafutia watu mbalimbali kwa sasa.