Blogger Widgets

October 10, 2013

Majanga Mengine Yaliyomkuta Msanii Nora Baada ya Kuanzisha Kampuni Akiwa na Mpenzi Wake GeofreyUHUSIANO wa wasanii wawili wa filamu Bongo, Nuru Nassoro ‘Nora’ na Geofrey Kusila umeota mbawa baada ya kumwagana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.


Chanzo  kilicho karibu na wasanii hao kimepenyeza habari kuwa uhusiano wao umevunjika bila kufahamika chanzo.


“Nora na Geofrey wameshaachana na kila mtu ana maisha yake hata kazi hawafanyi tena pamoja, tangu walipoachana Nora anaandaa kipindi chake  kwenye runinga na hayupo tena na Geofrey,” kilisema chanzo hicho.


Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwandishi wetu alimtafuta Nora ili kuujua ukweli, akafunguka:
 

“Mimi ninafanya kazi zangu mwenyewe na Geofrey kivyake kwa sababu tumeachana na kampuni ambayo tulikuwa  tumeianzisha nayo imekufa na baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake na kuangalia jinsi gani atakavyofanya kazi hivyo hatupo pamoja tena.”