Blogger Widgets

October 15, 2013

Miujiza:Shuhudia Picha Mtoto aliyekuwa kafariki na Kuombewa Mpaka Kufufuka Huku Arusha


Mtoto aliyefufuka (katikati) akiwa ameshikwa na Mch. Gwajima (kulia) na Mch. Costa (kushoto)

Ni jumapili tulivu katika viwanja vya kanisa jipya la Ufufuo na Uzima jijini Arusha; ambapo
Mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Tanzania, Mch. Josephat Gwajima ameendelea na ziara yake mkoani humo kwa kuwafundisha viongozi wapya wa masomo ya kumtumikia Mungu maarufu kama Potential shepherd. Mwisho wa Ibada ya Asubuhi ambayo ilitawaliwa na mafundisho zaidi ilifungua pazia kwa ibada ya jioni ambayo ilikuwa ni fursa kwa wale ambao hawakuweza kuwepo asubuhi nao kushiriki.

Majira ya saa kumi kamili, sifa zilivuma na baadaye kufuatiwa na ukaribisho wa Mch. Gwajima kutoa neno la Uzima. majira ya saa kumi na mbili kasoro; akaingia mama mmoja katikati ya ibada akiwa amembeba mwanaye ambaye kwa muonekano wa awali alikuwa amelegea mwili wote yaani amekufa.
Mama huyo ambaye alikuwepo katika mafundisho ya asubuhi na kujiunga na mafundisho hayo ya potential shepherd; aliendelea kusema kuwa baada ya kuona mwanaye hapumui wala mapigo ya moyo hayasikiki hakuona msaada wa haraka zaidi ya kumkimbiza kanisani hapo Ufufuo na Uzima.




Aliingia kanisani wakati Mch. Josephat Gwajima akiwa anahubiri hivyo kupokelewa na Mchungaji Msaidizi aitwaye Yeconia Bihagaze ambaye alimuombea mtoto huyo palepale na muda mfupi uliofuata mtoto alifufuka kutoka kwa wafu. Mungu ameendelea kudhihirisha neno la Mchungaji Josephat Gwajima ndani ya jiji la Arusha hali inayosababisha maelfu ya watu kuingia na kutoka katika viwanja hivyo kwaajili ya maombezi.


Jackson Benty akiimba katika ibada kanisani hapo.
Hata hivyo GK ilipotaka kupata maelezo zaidi kuhusiana na mambo yalivyokuwa mpaka mtoto huyo kufikishwa madhabahuni, mwanahabari wetu kutoka Ufufuo hakupata nafasi ya kukutana na mama huyo kwa maelezo zaidi kutokana na mwanahabari wetu kutingwa na kazi nyingi za media kanisani hapo.


Mchungaji Gwajima akifundisha kanisani hapo. Picha na shuhuda zaidi tembelea


 

No comments:

Post a Comment