Blogger Widgets

October 24, 2013

Nando Ala Dili Lingine Ndani ya BBA Mwaka 2014


Ammy Nando ambaye alituwakilisha mwaka huu katika shindano la Big Brother Africa, The Chase amepata nafasi ya kutuwakilisha tena katika shindano hilo hapo mwakani 2014. Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika katika Ofisi za Multi Choice Tanzania zimethibitisha hilo. Nando alikuwa disqualified na kutolewa katika shindano hilo mwaka huu baada ya kugombana na kutishia kumchoma
kisu mshiriki kutoka Ghana anayejulikana kama Elikem. Sasa sijui jamaa kajirekebisha na hataleta fujo tena???? Habari za uhakika zinathibitisha kuwa Nando amekubali offa hiyo na yuko tayari kwenda kuipeperusha bendera ya Tanzania tena.......