Blogger Widgets

November 16, 2013

Tazama Kizaazaa KIlichozuka Baada ya Irine Uwoya Kuweka Majibu yake ya HIV Hadharani

Majibu ya ukimwi ya mwanadada Irene Uwoya yamezusha vuta nikuvute huko kwenye mtandao maarufu wa kijamii   wa picha na video nchini baada ya shabiki mmoja wa Irene uwoya ‘kum-diss’ mwanadada huyo kuwa hayo majibu si kweli labda kama ni majibu  ya vipimo vya ugonjwa wa Malaria kwa maana kuwa hakubali na haamini kama Irene uwoya anweza kuwa HANA ugonjwa huu wa kisasa kutokana na sababu zake binafsi anazozijua shabiki huyo ambazo sisi tumeshindwa kuzifahamu mpaka sasa.

Ilikuaje?
Mwanadada Irene Uwoya aliamua kuweka majibu ya vipimo vyake hivyo vya gonjwa hili hatari sana kama njia ya kuwashauri watu waende kupima kwa kufuata mfano wake yeye kama kioo cha jamii

Maoni ya mashabiki yakaanza…
Muda mfupi tuu baada ya mwanadada huyo kuweka majibu ya vipimo vyake hivyo yanayoonesha kuwa mrembo wetu huyu yupo NEGATIVE ama hana maambukizi ya ugonjwa huu ndipo watu mbalimbali walipoanza kutoa maoni hayo kuhusu majibu hayo.

Mtafaruku…
Baada ya muda kidogo ndipo baadhi ya mashabiki walipoanza kuhoji uhalisia wa majibu hayo kwa kuanza kuuliza maswali kama:
Asina : “Mbona haijaoneshwa km ni HIV?”
Salm: “Hhhhhmm Mamaa tarehee iko wapi?”
Na ndipo huku wa tatu alipogusa mtima wa Irene kwa kauli yake la utata kuhusu majibu hayo na kulianzisha sakata hilo;
Lulu: “Hongera kwa kua huna malaria bt ngoma ustake tuumbuane”

Irene amjibu….
“Inawezekana nilitembea na…… (Manaeno ya hapa yamefutwa kutokana na sababu za kimaadili)”  huku akimlenga huyo mwanadada anayeitwa lulu aliyetoa hoja yake hapo juu

Udakuzi waanza….
Jacq:  “Asante kwa jibu zuri ulilompatia huyo kiumbe coz kuna watu hawanaga vya kucoment yan ilimradi tuu na yy kacoment!!#watanzania tubadilike khaaa...big up kipenz…”
Mbalumimi??: “Jibu limejitosheleza kuna watu wamezaliwa na vijiba kha”
Glyn:  “lulu umelipata likufaalo buhaha”
Makii: “Jibu kwa mtu kama wewe tena kioo cha jamii... ukweli hapana. Wasanii ijueni nafasi yenu kwenye jamii…”
Salmin: “Mamaa usifanye tena hivyo, ww ni SomeHoney kwa Tanzania na wengine ni Some1,jaribu kuplay part yako Usijibu jibu 2, Unashusha dat ID n CV of yars 2nakuchallenge hw far cn u go....”

Aliyelianzisha naye aongea tena….
Lulu: Sikumaanisha vibaya kusema hivyo...irene na huna sababu ya ku?panick hivyo anyway asante kwa kunikumbusha kuwa baba yangu ni marehemu... majibu mnayoyatoa yanaweza yakakufanya watu wajue ukoje... nimekujibu kistaarab coz sina ubaya na wewe but the next time kabla hujanijibu pumba zako tafakari comment n ujibu.

Irene uwoya ampa jibu zito tena….
Irene Uwoya: “Tena ukome kama uwez ku comment vizuri acha pia....minimeweka chet changu unaongea pumba wakat napima ulikuwepo?maana unaongea kama vile umewah kunipima....kumbe vinauma...poleeee” Sina mda na mwezi mchanga

Naye Irene apewa jibu zito safari hii…
Lulu: Siumii kabisaa ndo maana niko relaxed ninavyo kujibu.... wee ndo una pressure relax mamaa siumii hata kidogo maskini pole sana jifunze kutafakari vitu u big time(Tusi) ungeelewa comment ya kwanza haya yasinge tokeaaa!

Irene Uwoya atumia busara zake kuomba radhi.
Irene Uwoya: Yan wapenz wangu polen kama nimewauz...mi nimeweka chet nakuwashauri tuuu...lakin naona kuna watu wanataka kufanya wananijua sana

Huyu aamua kuwatuliza  yaishe….
Jose: Basiii!!!inatosha usiku sasa jamani,@PIPOOO,kwani nyie madokta? Ok kesho ntamchukua cc Irene na gari la PA tumpime hadhari muache kuongea,,MSIPENDE BISHANA BANA,,#life ni fupi joooooo,so baaabaabaaa banjuka tu,co kutupiana maneno# NANYI MKAPIMEEEEEEE!!!
Mmmh! Kweli ustaa kazi