Blogger Widgets

November 18, 2013

Tazama Picha Huyu Msanii wa Bongo Movie alivyopata Pigo na Kusababisha Kulia kwa Uchungu Mbele ya Umati

Mike Sangu akilia kwa uchungu baada ya kuondokewa na dada yake.
 Msanii maarufu wa sinema za Kibongo, Michael Sangu ‘Mike’ amepata pigo la kuondokewa na dada yake, Salma Said na kujikuta akilia kama mtoto mdogo na kusababisha watu kuwa na kazi ya ziada kumbembeleza.

 Mike alipatwa na pigo hilo wiki iliyopita baada ya dada yake huyo kuugua kwa muda mfupi akisumbuliwa na maumivu ya titi moja lililokuwa limevimba hali iliyosababisha kifo chake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar.


“Naumia sana, dada yangu alikuwa kila kitu kwangu kwani alikuwa akinishauri mambo mbalimbali kuhusu maisha, ukweli ameniachia pengo kubwa sana ila ndiyo mipango ya Mungu nitafanyaje,” alilalama Mike kwa uchungu.

Mazishi ya dada huyo yalifanyika Ijumaa iliyopita katika Makaburi ya Kinondoni, Dar na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo waigizaji wa filamu ambapo  mkewe, Salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ alikuwa na kibarua kizito cha  kumbembeleza Mike anyamaze.