Kuna taarifa kuwa Watanzania wawili wamekamatwa na dawa za kulevya nchini India na kwamba mmoja wao amefariki dunia. Taarifa zinadai kuwa Watanzania hao, ambao walikuwa watatu, waliwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Chatrapati Shivaji juzi asubuhi na Ethiopian Airlines Flight 610.

Baada ya kutua uwanjani hapo, maafisa kutoka uwanjani hapo waliwakamata Watanzania wawili kati ya watatu kwa mahojiano zaidi baada ya kutonywa (tip-off) kuwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Baada ya kuhojiwa kwa muda wa masaa matano, Watanzania hao walikataa katakata kuwa walikuwa "punda" wa dawa za kulevya.


Taarifa zinadai kuwa maafisa hao waliamua kuwapa Watanzania hao chakula na maji kama trick ya kujua kama walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Kwa kawaida, mtu aliyemeza vidonge vya dawa za kulevya hali wa kunywa ili kuepukana na kifo. Hivyo basi, kama mtuhumiwa akipewa chakula na kukataa kula inaweza kuwa ni dalili kuwa amemeza vidonge vya dawa za kulevya.Hivyo basi, baada ya kupewa chakula na maji, Mtanzania mmoja alikataa kula wala kunywa. Hata hivyo, Mtanzania wa pili alikubali kula chakula alichopewa. Baada ya hapo, Watanzania wote watatu walipelekwa mahakamani, lakini yule aliyekubali kula alikataa na kutaka kukukimbia. Baada ya purukushani katika eneo la mahakama, yule aliyekubali kula chakula alifariki baada ya kuzidiwa na vidonge vya cocaine kama 120 alivyokuwa amemeza.


Hali ya Mtanzania wa pili ilizidi kuwa mbaya na alipelekwa katika hospitali ya JJ. Baada ya kufanyiwa X-ray na CT-scan alikutwa amebeba vidonge vya cocaine kama 100 hivi. Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa hosipitali hiyo, hali yake ni mbaya lakini hajapelekwa ICU.


Mtanzania wa tatu, ambaye ni mwanamke wa makamo, bado anahojiwa na vyombo husika. Mwanamke huyo hakukutwa na dawa zozote lakini alikuwa ameongozana na wanaume hao wawili. Upelelezi bado unaendelea kujua kama alikuwa mmiliki wa hizo dawa za kulevya.


Habari kwa mujibu wa
India Today, The Times of India, Daily News India and Jamii Foroum