UCHUMBA wa staa wa wimbo wa Muziki Gani, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ na mpenzi wake
anayefahamika kwa jina moja la Siwema umedaiwa kuvunjika.Kwa mujibu wa
chanzo makini, chanzo cha kumwagana ni baada ya Siwema kukuta meseji za
watoto wa kike tofauti katika simu ya Nay wa Mitego katika nyakati
tofauti.
Chanzo hicho kimeeleza kuwa, wawili hao walimwagana tangu Januari 2,
mwaka huu, nyumbani kwa Nay wa Mitego, Manzese jijini Dar es Salaam
baada ya Siwema kujiridhisha kuwa mpenzi wake huyo anamsaliti kutokana
na ushahidi wa meseji alizozifuma.
Hata hivyo, chanzo kilizidi kumwaga ‘ubuyu’ kuwa, wapendanao hao
wamekuwa wakizinguana mara kwa mara na kilichomuuma zaidi Siwema ni
baada ya mkali huyo kuachia video yake mpya ya Nakula Ujana ambayo
ameonekana katika pozi za kimahaba na warembo kibao.
“Imemuuma sana video ya Nakula Ujana, warembo wale inasemekana hakuishia
katika video, sasa aliendelea kuwasiliana nao na Siwema akagundua ndipo
mtiti ulipoibuka, Siwema akarudi kwao Mwanza,” kilisema chanzo.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Siwema
ambaye alikiri kugombana na Nay na kusema ameshindwa kuvumilia na ameona
ili kujiepusha na presha zisizo za lazima arudi kwao Mwanza.
“Kweli tuna ugomvi na Nay na haswa kuna mambo yananikera sana ila kubwa
zaidi kwa sasa ni ile video yake mpya kuna parties mle
sijazipenda…mchumba wa mtu ufanye video ujiachie vile, unashikwa shikwa
ovyo,” alisema Siwema.
Alipotafutwa Nay, alikiri kutokea kwa ugomvi huo na kudai yupo katika
jitihada ya kumaliza tofauti hizo kwa kuzungumza na Siwema.
No comments:
Post a Comment