Masjid
Mussa, msikiti katika jiji la Mombasa,Kenya, ilikuwa Jumapili (tarehe 2
Februari) eneo la makabiliano mengine kati ya vikosi vya usalama vya
nchi na vijana wanaoshukiwa kuwa wenye siasa kali.
Ofisa wa polisi akielekeza kirungu kwa wanaume waliowekwa chini ya ulinzi nje ya Masjid Mussa huko Mombasa tarehe 2 Februari, 2014. [Na Ivan Lieman/AFP] |
Vikosi
vya usalama vilivamia jengo la msikiti Jumapili jioni katika
kukabiliana na kile kinachosemwa kilikuwa jitihada zilizopangiliwa za
kuandikisha vijana na kutoa mafunzo kwa vijana kwenye shughuli za
jihadi, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Mombasa Robert Kitur aliiambia
Sabahi.
Kati ya watu watatu waliouawa katika tukio hilo, mmoja alikuwa ofisa wa
polisi ambaye alikufa kutokana na majeraha ya visu, alisema, akiongezea
kwamba watu 200 walikamatwa katika mapambano hayo.
Kijana akionyesha ukaidi akiwa ameshikilia bango la jihadi baada ya kukamatwa katika eneo la Majengo la Mombasa tarehe 2 Februari, 2014. [Na Ivan Lieman/AFP] |
Mahakama
Jumatatu, iliagiza kwamba watu 129 waliokamatwa katika operesheni hiyo,
ikiwa ni pamoja na wanawake watatu, kuendelea kuwa chini ya ulinzi hadi
tarehe 7 Februari kutoa muda kwa polisi kukamilisha uchunguzi, Kitur
alisema.
Vijana wa kiume wakiwa wamelala chini nje ya Masjid Mussa huko Mombasa baada ya kukamatwa tarehe 2 Februari, 2014. [Na Ivan Lieman/AFP] |
Wakati
vikosi vya usalama vikielekea msikitini, vilikutana na vijana wenye
silaha, mapanga na fimbo, wakikataa kuwaruhusu kuingia katika eneno
hilo, kwa mujibu wa Kitur. Alisema vikosi vya usalama vilivamia msikiti
huo baada ya vijana kukataa kutekeleza amri ya kujisalimisha na kuwapiga
risasi maofisa polisi.
"Tuliwanyang'anya visu, fimbo na bendera zinazohusiana na al-Shabaab.
Polisi walipanda kwenye minara kuondoa bendera zilizokuwa zikipepea,"
Kitur alisema, akiongezea kwamba iliwachukua vikosi vya usalama zaidi ya
saa tano kuweka hali ya usalama katika majengo manne ya jengo la
msikiti.
ABaadhi bya watu waliokamatwa wakati wa operesheni kwenye Masjid Mussa wakipelekwa mahakamani Jumatatu na vikosi vya usalama (tarehe 3 Februari) katika kitongoji cha Shanzu cha Mombasa. |
"Tulipata
habari za mkutano wa Alhamisi [tarehe 30 Januari] kupitia dokezo la
tahadhari kutoka katika jamii. Mkutano huo ulitangazwa pia kupitia
vipeperushi na vyombo vya habari vya jamii," alisema. "Tulitoa tahadhari
kwamba hatutaruhusu mkutano kama huo kwa sababu ni kinyume cha sheria."
Mkuu wa polisi wa
mkoa wa Pwani Aggrey Adoli alisema vikosi vya usalama vilikuwa tayari
kumaliza mara moja vurugu ili kuleta hali ya kawaida kwenye mji.
Alisema vikosi vya usalama vilikuwa katika tahadhari endapo mkutano na
ulinzi wa usalama unaofuatia ulikuwa ni hila za kuvizuia vikosi vya
usalama kutokana na mashambulizi ya al-Shabaab pengine popote.
"Mkutano wa watu wenye msimamo mkali ulikuwa ukiendelea tangu asubuhi.
Pia tunachunguza kwamba mkutano ulifanyika Ijumaa," aliiambia Sabahi.
"Tunaamini vijana walitaka kuleta hali ya vurugu idumu kwa saa au siku
kadhaa au hata miezi kuleta uzingativu. Vijana waliasi agizo la vikosi
vya usalama kuondoka bila ya masharti kwenye mkutano na kutawanyika."
Polisi walitaka kuutawanya mkutano kwa amani, na kuepuka kuwa na majeruhi na uharibifu kwenye sehemu takatifu, alisema.
Adoli alisema viongozi wa usalama wanapanga kufanya mkutano na wahubiri
wa Kiislamu katika mkoa ili kujadili hali inayoendelea. Sehemu ya ajenda
ya mkutano itakuwa kujadili uwezekano wa kufunga Masjid Mussa kwa
sababu ya kutumiwa kwake na vijana na wahubiri wenye msimamo mkali
kuleta vurugu nchini, alisema.
"Tunaamini kikundi cha wenye msimamo mkali kinatumia msikiti katika
kujaribu kuvutia utumiaji nguvu wa usalama ambao matokeo yake unavutia
upinzani dhidi ya vikosi vya usalama," alisema.
Katika kujibu uwezekano wa kufunga msikiti, Seneta wa Kaunti ya Mombasa
Hassan Omar Hassan alisema Jumapili kupitia Facebook, "Nina matumaini ya
dhati kwamba ripoti kama hizo sio za kweli kwa kuwa hakuna serikali
inayoweza kufanya tukio kama hilo la uvunjaji mkubwa wa sheria dhidi ya
dini yoyote. Kitakuwa ni kitendo cha uchokozi ambacho ninakipinga
kabisa."
"Ninawaomba viongozi wote na raia wetu wote wa Mombasa kutumia jitihada
zetu nzuri ili kutafuta suluhisho kwa masuala haya," alisema, akiongeza
kwamba suluhisho "lazima lipatikane kwa uhusishaji na majadiliano".
Masjid Mussa unafahamika kwa kusambaza msimamo mkali na unajulikana
kufuatwa mara kwa mara na wafuasi wa marehemu Aboud Rogo Mohammed
aliyeuawa kwa kupigwa risasi akiendesha gari mwezi Agosti 2012, tukio
ambalo lilichochea siku kadhaa za vurugu Mombasa.
Rogo na wafuasi wake mara nyingi walitumia msikiti kama mahali pa
kutolea hotuba, mahubiri na mihadhara kuhusu uadilifu wa jihadi.
Uvamizi wa Msikiti wasababisha Kero
Abdi Mwashumbe, 34, mkazi wa Mombasa, alisema alikuwa ndani ya msikiti
wakati makabiliano kati ya vijana na vikosi vya usalama yalipoanza.
Alisema wasiwasi ulianza kujengeka wakati maofisa wa polisi walipotumia
vipaza sauti kuamrisha waumini kuondoka msikitini huku wakiinua mikono
yao juu.
Amri zote zilifuatiwa na kundi la vijana ndani ya msikiti kukariri kaulimbiu za kidini, alisema.
"Baadhi ya waumini walikuwa hawajui kama mikutano ya wenye msimamo mkali
ilikuwa ikiendelea katika eneo hilo," Mwashumbe aliiambia Sabahi. "Wote
tuliokuwa hatuna taarifa ya chochote tulitaka kufuata amri ya polisi na
kutoka nje, lakini baadhi ya vijana ndani walitutaka tuondoke."
"Ilionekana kama hali ya mateka kwa sababu tulikuwa tukitumikia kama
ngao," alisema, akiongeza kwamba baada ya saa mbili alikuwa na uwezo wa
"kutembea kawaida na kupenya kimyakimya kutoka nje ya msikitini".
Mwashumbe alisema kwamba muda ya saa 9 alasiri, baada ya kuondoka, alisikia bunduki na mabomu ya machozi yakirushwa.
"Ninaamini polisi watawahoji kikamilifu wale waliowakamatwa kwa sababu baadhi yao hawana hatia," alisema.
Sheikh Abdallah Kheir, imam na mhadhiri wa sosholojia katika Chu Kikuu cha Kenyatta, alishutumu matumizi ya nguvu msikitini.
Alisema mkutano msikitini ulitangazwa kama mhadhara wa dini na polisi haikuwa na sababu ya kuuvuruga.
"Msikiti ni mahali patakatifu, lakini polisi waliingia msikitini wakiwa
na viatu vyao na kufyatua risasi zao na mabomu ya machozi ndani ya
msikiti," aliiambia Sabahi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya polisi, maofisa walifyatua silaha zao nje ya msikiti.
Kheir alisema serikali inapaswa kushughulikia msimamo mkali kwa kutoa fursa kwa vijana.
"Vijana wengi hawana cha kufanya na wapo hatarini kwa wanaitikadi ambao
wanabadilisha mawazo yao. Serikali pia inahitaji kushughulikia uonevu wa
kihistoria na kutengwa kwa vijana katika mkoa wa Pwani," alisema
No comments:
Post a Comment