Blogger Widgets

March 21, 2014

Moja ya habari inayozungumziwa ni hii ya msanii wa kike wa bongomovie "SHUMILETA"

Huku kukiwepo na madai ya baadhi ya mastaa wa Bongo kwenda nchi za nje kufanya biashara ya kujiuza, siri imevuja kuwa, staa wa filamu aliyepotea kwenye soko la filamu Bongo, Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’ amedaiwa kumuuza msanii mwenzake wa kike, Lungi Maulanga kwa mwanaume aishie nchini India.
Lungi Maulanga.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mchongo huo ulifanyika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya Shumileta anayesaka maisha nchini humo kuona picha ‘sex’ ya Lungi , fasta akamtafutia mteja, raia wa Nigeria (jina kapuni).
Baada ya kumegewa mchapo huo, waandishi wetu waliingia mzigoni na kufanikiwa kunasa mawasiliano ya msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga na Shumileta kupitia mtandao wa Instagram. 
‘Charting’ hizo zilionesha ‘live’ kuwa Shumileta amemuomba Lungi amtafutie bwana huyo wa Kinaigeria, akafanikiwa kuwaunganisha na wakaanza kuchati kupitia Mtandao wa WhatsApp ambapo mwanaume huyo alimuahidi Lungi mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kumtumia picha yake.
Staa wa filamu za kibongo Jennifer Mwaipaja ‘Shumileta’.
Lungi alipoulizwa na mapaparazi wetu juu ya mawasiliano hayo ya kibiashara alifunguka:
“Nyie mmepata wapi habari? Hiyo simu yangu ilipotea, nahisi mtakuwa mmeona mawasiliano yangu humo. Kwani Shumi kunitafutia bwana kuna tatizo gani? Bwana kaniona, kanipenda na mimi nimechati naye, kuhusu mambo ya kwenda Naigeria hiyo haiwahusu.” 
Ili kuleta usawa wa habari, mapaparazi wetu walimtafuta Shumileta kwa njia ya simu, mambo yalikuwa hivi:
Mwandishi: Shumileta mambo vipi?
Shumileta: Safi, niambie.

Lungi  Maulanga.
Mwandishi: Tumepata habari kuwa umemuuza Lungi kwa mwanaume Mnaigeria huko India?
Shumileta: Aliyekwambia nani? Mfuate muulize vizuri, mimi sizijui hizo habari.
Mwandishi: Mbona lakini kuna SMS zako zimefumwa kwenye simu ya Lungi ukimtafutia bwana?
Shumileta: Mfuate kamuulize mwenyewe.

No comments:

Post a Comment