Blogger Widgets

July 22, 2012

HII SI HADITHI LAKINI NDIVYO VUNJA JUNGU YA MACHANGU ILIVYOKUWA



Stori: Issa Mnally na Richard Bukos
KATIKA hali ya kushangaza, usiku wa Jumanne iliyopita, Risasi Jumamosi liliwanasa akina dada wanaojiuza ‘machangudoa’ ambao walisema hawatakuwepo katika eneo la biashara kwa muda wa mwezi mmoja kwa sababu ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.



Machangu hao walinaswa Corner Bar, Africana Sana- Sinza, jijini Dar es Salaam ambapo walikuwa wakisaka wanaume huku wakidai wanavunja jungu.
Akizungumza na mapaprazi wetu, Rose aliyedai ni kahaba mzoefu wa eneo hilo alisema mara mfungo utakapoanza hata wao watasitisha biashara hiyo mpaka watu wenye imani hiyo watakapomaliza ibada yao.

Unajua nini? Ni kweli tunatenda dhambi, lakini sasa si vizuri wenzetu wafunge halafu sisi tunashughulika na zinaa kwa kuuza mwili, hata Mungu hapendi. Kwa hiyo mimi nitaacha ili kuungana na wenzetu,” alisema Rose, mwenyeji wa Mbeya.

                                          SOURCE: From Global Publisher

No comments:

Post a Comment