Blogger Widgets

January 3, 2013

Taadhali yatolewa na Mwenyekiti wa kamati ya Mazishi ya Marehemu Sajuki Kuhusu mtu Feki anaejinadi kwa kuchangisha Fedha za Mazishi kwa Njia ya simu

wastara




Kwa mujibu wa Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia jana, kumejitokeza watu wanaojifanya kutumwa na familia kuchangisha fedha kwa njia ya simu.
Steve amesema kuna mtu mmoja anayetumia jina kubuni Tumaini ameendelea kukusanya fedha nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na kusema kuwa waache mara moja kwakuwa ni mwizi.

Steve amekielezea kitendo hicho kama wizi usio na aibu kwa familia ya Sajuki iliyopo kwenye majonzi makubwa.Ameongeza kuwa taratibu zote za kukusanya fedha zinaendelea msibani maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam huku yeye na Mike Sango wakihusika na ukusanyaji huo.
MATUKIO YA MSIBANI



Pichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya 
Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba 
akipata maelezo mafupi kutoka kwa Rais wa  Shirikisho la 
Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba (wa pili 
kushoto) kuhusiana na mikakati na mipango mbalimbali ya 
mazishi ya Marehemu Sadick Juma Kilowoko a.k.a 
Sajuki,nyumbani kwao Tabata Bima,jijini Dar.Aidha kwa 
taarifa rasmi kutoka kwa Simon Mwakifwamba ameeleza 
kuwa mazishi ya marehemu yatafanyika kwenye makaburi ya
 Kisutu siku ya Ijumaa mapema saa tano asubuhi.Kuli kwa 
Naibu Waziri ni Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds Media 
Group,Ruge Mutahaba.na Rais wa  Shirikisho la Filamu 
Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akitoa maelezo 
mafupi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi 
na Teknolojia,Mh January Makamba kuhusiana na taratibu 
mbalimbali kuhusiana na msiba huo,huku baadhi ya wasanii 
wengine mahiri wa filamu wakisikiliza kwa makini.
 Mazungumzo mengine ya hapa na pale yakiendelea kufanyika kuhusiana taratibu nzima za msiba wa Sajuki,ulioko Tabata Bima,jijini Dar.

Rais wa  Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba,kushoto ni Mkurugenzi wa utafiti wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba.
 Baadhi ya Wasanii wa wakijadiliana jambo.
 Dua ikiendelea kusomwa nyumbani kwa marehemu Sajuki.
 Baadhi ya Watu mbalimbali wakiwemo wasanii wakongwe wa filamu wakiendelea kuwasili nyumbani kwa marehemu Sajuki mapema leo jioni. 
Watu mbalimbali wakiwe wenye simanzi kubwa wakijadiliana jambo
  
  Watu mbalimbali wakiwa wamekusanyika kwenye msiba wa marehemu Sajuki jioni ya leo maeneo ya Tabat Bima,jijini dar.
 Mdau mkubwa wa Filamu hapa nchini Saimon Simalenga akijaribu kutoa maelekezo mafupi kwa baadhi ya waombolezaji waliofika kwenye msiba wa marehemu Sajuki mapema leo jioni.
 Badhi ya Wadau na Wanahabari wakiwa wamekusanyika kwenye msiba huo.
Ruge Mutahaba akisalimiana na Mkurugenzi wa ASET,Asha Baraka,pichani kati ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia,Mh January Makamba pamoja na Simon Mwakifwamba.
 Wakifarijiana.
 Vikao vikiendelea
 Ruge Mutahaba akiwa ameongozana Mh January Makamba wakisalimiana na baadhi ya watu waliokuwa kwenye msiba,walipokuwa wakiwasili

Baadhi ya Wasanii wakibadilishana jambo
Source:Bongo5