Mwandishi wetu, Songea
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Songea wameiomba Serikali
kuwaongezea ulinzi kutokana na kufanyiwa vitendo vya kubakwa kimazingara
nyakati za usiku.
Dada
Mkuu wa Wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Songea Janemary
Mwinyikombo amesema tabia ya kuingiliwa kimwili mara mara na wanaume
imeongeza hofu ya wanafunzi na kusababisha wanafunzi kushindwa kujisomea
nyakati za usiku.
Janemary
Mwinyikombo akiwa na Katibu wa wanafunzi Bernadetha Mathew Pamoja na
Wanafunzi waliofanyiwa vitendo vya kinyama ikiwa ni pamoja na kuchaniwa
nguo kwa wembe na Mwanaume ajulikanaye kwa jina la Ankol ambaye mara kwa
mara huingia kwa njia ya kimazingara wamesema hali hiyo inawakosesha
raha shuleni hapo
Wamesema
pamoja na wanafunzi kufunga milango na kupigilia misumari kwenye
madirisha lakini cha kushangaza wanaume hao huingia na kuchana nguo za
wasichana maeneo ya kifuani na sehemu za siri.
Rosemary
amesema hali hiyo hutokea kuanzia saa saba usiku ambapo wanafunzi hao
hukumbwa na hali ya kushindwa kusema pindi mwanaume huyo anapoingia
bwenini.
Hata
hivyo wameomba jamii na wazee wa mila kukaa na kuweza kulitatua tatizo
hilo vinginevyo itasababisha wanafunzi kuathirika zaidi kisaikolojia
jambo litakalo sababisha elimu kuporomoka shuleni hapo.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo Welinald Riki Liwiki amekiri kuwepo kwa Vitendo
hivyo na amesema ameongeza ulinzi, yeye mwenyewe pia anashiriki ulinzi,
ameomba Jamii kushirikiana na shule katika kuwafichua watu wanaofanya
vitendo hivyo kwa wanafunzi.
“Nimekuwa
nikishiriki katika ulinzi wa usiku na nakumbuka siku moja nilinusurika
kuuwawa na mlinzi wetu baada ya kudhani mimi ndiye mwanaume anaye
waingilia wanafunzi kimazingara” amesema Liwiki
Shule
ya Sekondari ya wasichana Songea kwa miaka miwili mfululizo kumekuwa na
vitendo vya wanaume kuwaingilia wanafunzi kimazingara hali inayowafanya
wanafunzi hao kuishi kwa wasiwasi na kukosa umakini wa kusoma shuleni
hapo.
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment