Blogger Widgets

August 8, 2012

HUYU NDIO NAIBU WAZIRI WA VIJANA ALIYETOA VIDEO YA NGONO NA KUSIMAMISHWA KAZI

Waziri Atoa Video ya Ngono, Afukuzwa Kazi

NewsImages/6561950.jpg
Karina Bolanos, mwanamama aliyekuwa akishikilia nafasi ya unaibu waziri wa vijana nchini Costa Rica
Wednesday, August 08, 2012 1:53 PM
Naibu waziri wa vijana wa nchini Costa Rica amepoteza kazi yake baada ya video yake ya ngono kuvuja kwenye mitandao online.
Karina Bolanos, mwanamama aliyekuwa akishikilia nafasi ya unaibu waziri wa vijana nchini Costa Rica, amepoteza kazi yake baada ya kusimamishwa kazi pale video yake ya ngono ilipovuja online.

Katika video hiyo, naibu waziri huyo anaonekana akiwa amevalia nguo za ndani tu akipanda kitandani akijizungusha zungusha huku akitoa maneno ya kimahaba kumuita mwanaume wake apande kitandani.

Wizara ya utamaduni na vijana ya Costa Rica ilitoa taarifa kuwa kitendo cha naibu waziri huyo kimemfanya asistahili kuendelea kukaa madarakani.


Katika kujitetea kwake, Karina alisema kuwa video hiyo ilirekodiwa miaka michache iliyopita na ilivujishwa online na mhandisi wa kompyuta aliyejaribu bila mafanikio kumchuna pesa naibu waziri huyo ili asiirushe hewani video hiyo.

Tukio la kusimamishwa kazi kwa naibu waziri huyo ni pigo jingine kwa rais mwanamke wa Costa Rica, Laura Chinchilla ambaye amekumbwa na idadi kubwa ya kujizulu kwa mawaziri wake tangu alipochukua madaraka miaka miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment