Blogger Widgets

September 2, 2012

Haya ndio maajabu aliyoyafanya Diamond Platnum kwenye live show ya DMV WASHINGTON


Diamond aka Platinum akiwapagawisha watanzania wapenzi wa music wake, Diamond aliimba nyimbo zake zote za zamani na mpya ambazo hata hazijaanza kusikilizwa  katika radio stations za Tanzania hapa akiimba kwa hisia moja ya nyimbo zake ukumbini hapo.
Hapa alivyo kuwa bado na vazi lake nazifu kabla ya mzuka kupanda na kutoa nguo hizo za juu.
Diamond kwa kushirikiana madancer wake walifanya show ya kuvutia sana na watu wote walifurahi na wangekuwa na uwezo wangetaka show hiyo kuendelea hadi asubuhi lakini wapi muda ukivyofika watu walijivuta kwa unyoge kwani waliona kama walikatizwa uhondo wakuendelea kupata burudani kutoka kwa Diamond na madancer wake.
Diamond akiimba kwa hisia na nyuma ni madancer wake
Walionyesha miondoko ya kiusafi usafi kama Diomond mwenyewe anavyojiita yeye ni rais wa wasafi kwa kweli walikuwa kivutio ukumbini hapo.



Watu wakifatilia kwa makini kabisa show ya Diamond ukumbuni hapo kama unavyo ona 





No comments:

Post a Comment