Blogger Widgets

October 25, 2012

Hii Ndio sababu iliyoonesha Rais wa Manzese Madee Kujitoa Tip Top





MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya anayewakilisha pande za Manzese, Hamad Ally ‘Madee’, kutoka kundi la Tip Top Connection, inadaiwa kuwa amejitoa katika kundi hilo, na sasa anataka kufanya muziki kivyake na sababu za kujitoa kwake bado hazijulikana.

Chanzo chetu cha habari kilichozungumza na DarTalk, kwa sharti la kutotajwa kwa jina lake kilidai kuwa wiki iliyopita msanii huyo alikuwa kwenye mzozo na mmoja wa wasanii wa kundi hilo lakini waliweza kupatana ingawa jamaa bado anaonekana kutopenda kile kilichotokea lakini bado kuna vitu vingine vya ndani zaidi vilivyosabisha hadi jamaa kuamua kujiweka pembeni.


Chanzo hicho kilichopo karibu na wasanii hao hakikusita kueleza kuwa ndani ya kundi hilo kuna matatizo mengi, kwani hata kuondoka kwa baadhi ya wasanii waliokuwa hapo sababu hizo ndiyo zimemfanya Rais huyo manzese kujiengua, ingawa bado kuna mvutano mkubwa unaoendelea ili kumrudisha kundini jamaa huyo bila taarifa za mkwaruzano huo kutoka nje.
   KWA HISANI Ya:  MPEKUZI

No comments:

Post a Comment