Katika hali
isiyo ya kawaida Kanisa la Moraviani Usharika wa Tunduma, juzi ilibidi
lisitishe kwa muda ibada, baada ya msichana mmoja Tumaini Mbembela (18) ambaye
ni mama lishe mjini hapa, kukutwa ameficha simu ya muumini mwenzake katika
kitenge cha kumbebea mtoto wa aliyemwibia.
Tukio hilo lilitokea Jumapili katika ibada ya kawaida iliyokuwa ikiongozwa na mchungaji wa kanisa hilo Atumigwe Msokwa,mara baada ya kuwaruhusu waumini wake wafanye toba kufuatia mahubiri yaliyotolewa na Mwinjilisti Bumijael Mshana.
Watu walioshuhudia tukia hilowalidai kumuona msichana huyo akiangaika kuificha simu hiyo , aina ya TECNO yenye thamani y ash.50,000 mali ya Mboka Petre (26) mkazi wa eneo la Kaloleni mjini hapa.
Akizungumzia hali hiyo Mboka alisema mtuhumiwa huyo alikuwa amekaa kiti kimoja na alianza kufnya zoezi la kumzoea kwa kumbeba motto wake Daniel Jafert (miezi mitano) hatua ambayo ilimfanya kutokuwa na wasiwasi naye hivyo alijikuta ameweka peupe simu yake..
Alisema baada ya kugundua kuwa simu yake haipo alipoiweka alimnongoneza muhudu mmoja wa kanisani hapo ambaye alitoa taarifa kwa mchungaji.
“Mchungaji alichukua uamuzi wa kutangaza kuibiwa kwa simu hiyo kisha alisimamisha shughuli za kutoa sadaka na kuwaomba wote waliokuwa katika foreni wasimame walipo.
Mchungaji Msokwa akizungumzia tukio hilo katika ibada hiyo alisema alipopata taarifa ya wizi huo alisitisha zoezi la kutoa sadaka lililokuwa likiendelea kanisani hapo na kiwataka waumini waliokaa katika kiti hicho akiwemo mtuhuniwa huyo wasimame.
Hatua hiyo ilimpa fursa mchungaji huyo kuanza kuwaita kundi la maombezi pamoja na aliyeibiwa simu kufika madhabauni tayari kwa ajili ya kuombea tukio hilo,kwa imani ya kupata jibu kutoka kwa Mungu..
Suhuda Diana Mlimakithi (15) alisema wakati hali hiyo ikiendelea, alimuona mtuhumiwa akihangaika kuficha simu hiyo kupitia kitenge cha kumbea mtoto huyo aliye achiiwa mtuhumiwa huyo , baada ya mama yake kuitwa na mchungaji kwa lengo la kutoa maelezo mbele ya waumini.
Kitendo hicho kilitoa mwanya wa mtuhumiwa huyo kuangusha simu aliyokuwa ameificha katikatiti lake la kushoto wakati akishuhudiwa na badhi ya waumini wengine akidondosha simu hiyo kwa ujanja.
Baada ya tendo hilo waumini walisemsimu hiyo imepatikana baada ya Tumaini kuidondosha hatua iliyompa nafasi mchungaji kuwaita wazee wa kanisa na kufanya mashauriano katika ofisi yake.
Akizungumza na gazeti hili Tumaini alikiri kuiba simu hiyo ushuhuda ambao aliutoa pia mbele ya waumini wa kanisa hilo huku akiomba msama kuwa tendo hilo hajawahi kulifanya tangu kuzaliwa kwake.
Baada ya tukio hilo Timu ya waombaji walimuombe msichana huyo ambaye wakati wa maombi hayo alidondoka na damu ilianza kumtoka katika baadhi ya maeneo ya mwili wake.