Blogger Widgets

May 16, 2013

Happy Birthday AD Plus,Baba la Baba,Adam Mchomvu,The People Poor Presdent,Hiki Ndio Kitakacho Happen Kwenye XXL BABY!!!

941722_10151432613846139_386016264_n


Mtangazaji wa vipindi vya XXL na Bongo Flava vya Clouds FM na rapper, Adam Mchomvu leo anatarajia kuachia mixtape yake aliyoipa jina, Baba Jonii Vol 1.
Adam ameichagua siku hii kwaajili ya kuzindua mixtape yake kwakuwa ni siku yake ya kuzaliwa.
“Kiukweli kabisa sio kwa maujanja yangu nimeweza kupenya na kufika mpaka hapa nilipo ni kwa uwezo wa Mungu na upendo wa family, marafiki, ndugu zangu na nyie wote kwa ujumla kila mmoja kwa nafasi yake ameniwezesha mimi kuwa mimi na kuwa hapa nilipo,” ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

“Ahsante sana kwenu kwa Amani na Imani kubwa mnayonipa duniani nazidi kupiga hatua, sina cha zaidi cha kuwapa ila naomba muipokee mixtape kama zawadi yangu kwenu, tu review track kadhaa kwa XXL baadaye sana tu.”