Blogger Widgets

May 16, 2013

Unalijua Hili Kuhusu Huyu Demu anayewakilisha Kundi la Camp Mulla Babyy!!!

Miss Karun


Habari zilizosambaa katika mitaa ya area code +254 zinadai kuwa kundi la hip hop lenye mafanikio makubwa nchini Kenya, Camp Mulla limempiga chini first lady na lead singer wa kundi hilo, Miss Karun.
Kwa mujibu wa maneno ya mtaa inasemekana nafasi ya Miss Karun itachukuliwa na mrembo mwingine aitwaye Tiri, ambaye ni mpenzi wa member na producer wa kundi hilo K’cous.
Siku chache zilizopita kulizuka uvumi wa uwezekano wa members wa kundi hilo kuendelea na solo projects kwa kila mmoja wao ifikapo mwezi June 2013, kitu ambacho kinafanya tetesi za Miss Karun kuondolewa kundini kuchukuliwa kama dalili za kuvunjika kwa kundi hilo.

Camp Mulla wanategemea kupanda kwenye jukwaa moja na Snoop Lion katika concert ya MTV all stars Kwa Zulu-Natal hivi karibuni nchini Africa Kusini, show ambayo watampandisha mrithi wa Miss Karun kwa mara ya kwanza. 
From:Bongo5