Blogger Widgets

July 29, 2013

Icheck Pete Aliyovaaa Nick Minaj Inayosadikiwa Kuwa Kuvushwa na Dj KhaleedBaada ya Dj Khaled kutokea MTV akitangaza mapenzi yake ya dhati kuhusu nia ya kumuoa Nicki Minaj, mrembo huyu wa Young Money ameonekana Crustacean Restaurant Los Angeles Marekani akiwa na pete ya uchumba kwenye mkono wake wa kushoto wakati alipotoka kula chakula cha jioni na baadhi ya marafiki zake waliosoma pamoja High school.
Unadhani hiyo pete kavishwa na Khaled????!!! Biiig No…. kwa mujibu wa Necole hii ni pete ambayo inaaminika alivishwa na boyfriend wake wa longtime kitambo anaitwa Safaree ambae nae amekua akionekana kavaa pete kama hiyo ya gold ambayo imesababisha watu waamini pia uwezekano wa ndoa ya siri ya wawili hawa.Dj Khaled na huu mpango wake wa kutangaza nia ya kumchumbia Nicki Minaj aliiambia Power 106 kwamba anampenda sana Nicki Minaj kama ambavyo wanaume wengi wamekua wakivutiwa kumuoa pia, lakini akasisitiza kama Nicki atakataa kuchumbiwa na yeye… hakutakua na ubaya, bado ni marafiki…
Namkariri akisema ‘Nicki anaweza kutokua tayari kwa ndoa ila nitamwambia ninachofeel, hata akisema ndio kwangu au akiniahidi mwakani nitasubiri tu, sitokata tamaa… nataka watoto’


Rapper Rick Ross ambae ni rafiki wa wote Nicki Minaj na Dj Khaled ametoa baraka zake kama ni kweli hiyo ndoa ipo na miongoni mwa aliyoyasema ni uwezekano wa kuwapa gari kama zawadi ya harusi yao, mchek zaidi kwenye video hapa chini ambapo mpaka anahojiwa hapa alikua hajaiona video ya Dj Khaled akiomba uchumba kwa Nicki huku akiwa na pete mkononi.