Blogger Widgets

August 9, 2013

Vigogo Wawili waliokamatwa Dar Juu ya Kesi ya Agness Masogange Kuhusu Madawa ya Kulevya

HABARI zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Tanzania wakituhumiwa kumtuma Masogange kupeleka madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini
Kwa mujibu wa habari hizo, vigogo hao (majina tunayo) walidakwa wiki iliyopita kila mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar ambako walihojiwa kwa saa sita.
“Hawa vigogo walikamatwa wiki iliyopita na kuhojiwa kwa masaa sita, waliachiwa lakini waliambiwa wakihitajika tena wataitwa,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, vigogo hao, mmoja alinyang’anywa ‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti zake za benki zikifungwa kwa muda usiojulikana.
Habari zinasema kuwa, kigogo ambaye akaunti zake zimefungwa amekuwa akihaha kila kukicha kuhakikisha zinafunguliwa kwa sababu hana njia nyingine ya kuingiza kipato.
Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili kujua uhakika wa madai hayo ambapo alisema:
“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri kubwa, si rahisi kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa sababu mnaandika kwenye magazeti, matokeo yake uchunguzi unavurugika.
“Mfano wale wasichana (akina Masogange) waliokamatwa Afrika Kusini wamekuwa wagumu kuwataja waliowatuma kwa sababu hao waliowatuma ndiyo wanaowategemea kuwawekea dhamana.”
Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.